Mbowe angetakiwa kustaafu kwa manufaa ya Chama

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kwa taratibu za Chama hasa kwenye nchi za demokrasia Mh Mbowe angetakiwa kustaafu kwa manufaa ya uma. Waziri mkuu wa Canada ametangaza kustaafu sio kwasababu kashidwa uchaguzi lakini ni kwasababu viongozi wenzake wa ndani ya chama wamekosa imani kwake. Uingereza hii inatokea mara nyingi sana na ndiyo demokrasia.

Kama kiongozi umeamini agenda zako na hazija fanikiwa hasa kwenye Chama kwa utaratibu wa kawaida unapisha mawazo mapya. Sasa Mbowe sera yake ya Maridhiano kama kiongozi imeshindikana, viongozi wa Chama wanatekwa huwezi kusema kwa muhula huu wa miaka 5 Mbowe amefanikiwa. Kwasababu hiyo badala ya kupigania 51% busara za viongozi wengi hasa wa vyama wana staafu na kupisha agenda nyingine. Tumeona mara nyingi huko uingireza viongozi wa chama agenda zao zisiko fanikiwa au viongozi wengine muhimu wakikosa imani wanastaafu. Huwezi kuendesha chama kwa umakini kama huna support ya viongozi wengine. Kitendo cha viongozi ambao walimuunga mkono Mbowe 2019 na sasa hawamuungi mkono ni dalili tosha kwamba muda umefika. Tatizo la viongozi wengi wamezungukwa na wapambe ambao wanawakuza kuliko uhalisia. Kama hutakwi au watu wanafikiri mbinu zako hazijafanikiwa staafu usiwe kingangana. Mbowe ndiye aliyeenda kukutana na Samia na kumuamini kupiliza. Sasa matokeo yake ni kulipa huo uaminifu ambao ulimpa Mama

Kukosa imani haina maana kwamba Mbowe kahogwa au kapewa rushwa. Kukosa imani ni kutokumuamini tena hasa kwenye maamuzi. Mfano kwenye sekretati yake ya mwenyekiti manaibu katibu wakuu wawili wake zao wote ni wabunge wa viti maalumu ambao wapefukuzwa chama kwa kugushi nyaraka na bado wapo bungeni mpaka leo. Mbunge mwingine Mdee ambaye naye kafukuzwa ndiyo swahiba wako na mnakaribishana kwenye sherehe za kufunga mwaka. Sasa ni maamuzi ya Mwenyekiti lakini kwa mazingira haya huwezi kusema viongozi wengine kutokuwa na imanai na Mbowe wamekosea. Hao makatibu wakuu watawezaje kuwaunga mkono wagombea ambao hawataki wake zao waendelee kuwa wabunge!!!. Ndiyo maana ni busara Mbowe kustaafu kwa wenzake kukosa imani
 
Klabu ya Yanga ving'ang'anizi kama hawa 1980s tulikuwa tunawatoa Kwa bakora 😂😂
 
Inaonekana Timu Lissu inamuogopa sana Mbowe kwenye box la kura.
 
Mbowe anasema kina kitu amebakiza hajakimalizia akimaliza atastaafu.

Unajiuliza kitu gani ameshindwa kufanya kwa miaka 21, leo ndio aje afanye?

Sababu ya mbowe kukataa kustaafu ni moja tu, maburungutu kutoka kwa Abdul.
 
alichobakiza ndani ya chama labda ni kumuua LISu antipass mngwai
 
Back
Top Bottom