- Source #1
- View Source #1
Wakuu salama?
Nimekutana na hii kwamba Mbowe ameshauriana na familia yake na ameahidi kukata rufaa, je ina ukweli wowote hii?
Nimekutana na hii kwamba Mbowe ameshauriana na familia yake na ameahidi kukata rufaa, je ina ukweli wowote hii?
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alikiongoza chama hicho kwa takribani miaka ishirini. Uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho uliofanyika Januari 21, 2025 ulianzisha utawala mpya wa Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti akimshinda mshindani mkuu Mbowe aliyeondolewa madarakani.
Aidha uchaguzi huo uliofanywa na CHADEMA umetajwa kuwa ni uchaguzi uliozingatia misingi ya kidemokrasia kutokana na kuwa huru, haki na wazi. Mara baada ya uchaguzi huo kukamilika pamoja na kuhesabu kura kabla ya matokeo kutangazwa Mbowe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (Zamani twitter) alikubali kushindwa katika uchaguzi huo akimpongea Lissu. Hata hivyo Mbowe ataendelea kuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya chama.
Kumekuwapo na taarifa inayoonesha kuwa Mbowe aliahidi kukata rufaa mara baada ya kushauriana na familia yake dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo.
Je, uhalisia wa taarifa hiyo ni upi?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Mbowe hakuchapisha taarifa yoyote yenye nia ya kutaka kukata rufaa, katika ukurasa wa mtandao wa X wala mitandao mingine ya kijamii.
Aidha, Januari 22, 2024 ambayo ni tarehe inayoonekana katika chapisho hilo bandia, Mbowe aliandika ujumbe wa kukubali maamuzi yaliyofanywa katika uchaguzi wa mkutano mkuu wa CHADEMA huku akimpongeza Tundu Lissu kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la uongozi katika chama hicho.
“Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.”
Hata hivyo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na CHADEMA juu ya uwepo wa maombi ya mgombea yeyote ya kutaka kukata rufaa dhidi ya matokeo ya uchaguzi mkuu kwa nafasi ya mwenyekiti.