Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa tuhuma za kukiuka utaratibu wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Picha kwa hisani ya Jambo TV
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Augustino Senga amethibitisha kumshikilia kiongozi huyo pamoja na watu wengine 11.
Kamanda Senga amesema baada ya Mbowe kupokelewa uwanja wa ndege alitaka kuweka mkutano hapo hapo, jambo ambalo si sahihi kwa kuwa vyama vyote viliwasilisha maeneo ya mikutano yao.