Mbowe asikitishwa na wanaobeza maridhiano ya CCM, CHADEMA

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza kusikitishwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho kumfikiria kuwa anasaliti Watanzania kwa kufanya maridhiano ya kisiasa na CCM.

Akizungumza na wananchi leo Jumamosi Januari 21, 2023 wakati wa ufunguzi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho, Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kukubali maridhiano na hoja za Chadema.

“Yawezekana baadhi yetu msinielewe, namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan nimekaa naye kwenye vikao vingi vya kutafuta maridhiano.

“Yawezekana miongoni mwenu akanyanyuka yeyote kunikebehi, hatanipindisha msimamo wangu kwa sababu nachokisimamia kwa niaba ya nafsi yangu binafsi na kwa niaba ya Taifa hili, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

“Madam President alisimama kuiunga mkono hoja ya Chadema alafu nakutana na wanachama wa Chadema wanamuona alikosea, this is madness (huu ni uendawazimu),” amesema.

Amesema hatowafurahisha watu wanaotaka amtukane Rais Samia akisema kwa neno la kiingereza “I will never do that!”

Amesema wakati wanachama wakiona ugumu upande wa CCM kulikuwa na ugumu kuliko upande wa Chadema kwa sababu walijua maridhiano yoyote ya kisiasa wanakwenda kuiua na kuidumaza CCM.

“Nyinyi badala ya kunipongeza Mbowe mnakuja na mawazo ya kiharamia, Mbowe karamba asali hataki Katiba mpya hataki tume huru,” amesema.

Amesema walipoanza mazungumzo ya maridhiano moja ya misingi waliyokubaliana kuwa msingi wa mazungumzo hayo ni usiri, hivyo hata vuongozi wa Chadema walimuona akiingia na kutoka Ikulu bila kutambua kinachoendelea.

Pamoja na kumpongeza Rais, Mbowe amesema hataacha kuikosoa Serikali yake na maridhiano yao hayamaanishi vyama hivyo vitaungana bali Chadema itaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani nchini na baadaye kuwa chama tawala.

MWANANCHI
 
Bavicha Misifa mingi tu

Maridhiano hawataki na Maandamano hawawezi ni walegevu mno!
 
Wali ridhiana kuhusu nini, maridhiano huwa yanakuepo huko ambako hakuna amani wanapigana vita, sasa hayo maridhiano yalihusu nini hasa
 
Mlamba asali mkubwa
20230124_134832.jpg
 
Wanaolau yalipotangazwa maandamano walibaki nyumbani, hakuna sehemu youote duniani ilipata amani bila maridhiano, endelea Mbowe endelea, hawatakuelewa leo ila ipo siku watakuelewa.

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza kusikitishwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho kumfikiria kuwa anasaliti Watanzania kwa kufanya maridhiano ya kisiasa na CCM.

Akizungumza na wananchi leo Jumamosi Januari 21, 2023 wakati wa ufunguzi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho, Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kukubali maridhiano na hoja za Chadema.

“Yawezekana baadhi yetu msinielewe, namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan nimekaa naye kwenye vikao vingi vya kutafuta maridhiano.

“Yawezekana miongoni mwenu akanyanyuka yeyote kunikebehi, hatanipindisha msimamo wangu kwa sababu nachokisimamia kwa niaba ya nafsi yangu binafsi na kwa niaba ya Taifa hili, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

“Madam President alisimama kuiunga mkono hoja ya Chadema alafu nakutana na wanachama wa Chadema wanamuona alikosea, this is madness (huu ni uendawazimu),” amesema.

Amesema hatowafurahisha watu wanaotaka amtukane Rais Samia akisema kwa neno la kiingereza “I will never do that!”

Amesema wakati wanachama wakiona ugumu upande wa CCM kulikuwa na ugumu kuliko upande wa Chadema kwa sababu walijua maridhiano yoyote ya kisiasa wanakwenda kuiua na kuidumaza CCM.

“Nyinyi badala ya kunipongeza Mbowe mnakuja na mawazo ya kiharamia, Mbowe karamba asali hataki Katiba mpya hataki tume huru,” amesema.

Amesema walipoanza mazungumzo ya maridhiano moja ya misingi waliyokubaliana kuwa msingi wa mazungumzo hayo ni usiri, hivyo hata vuongozi wa Chadema walimuona akiingia na kutoka Ikulu bila kutambua kinachoendelea.

Pamoja na kumpongeza Rais, Mbowe amesema hataacha kuikosoa Serikali yake na maridhiano yao hayamaanishi vyama hivyo vitaungana bali Chadema itaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani nchini na baadaye kuwa chama tawala.

MWANANCHI
Lissu alipokuwa Nje ya Nchi kimatibabu nchi ilikuwa imezubaa sana ilibaki kidogo nchi iwe Zezeta.. Ila tangu Lissu arudi taifa limechangamka. Mambo yanapaswa kuwa namna hii ni haramu akili ndogo kuitawala akili kubwa.
 
Back
Top Bottom