Mbowe asirudie kupanda jukwaani akiwa amelewa, atatuaibisha zaidi

Mbowe asirudie kupanda jukwaani akiwa amelewa, atatuaibisha zaidi

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Hotuba ya Mbowe M/kiti wa Chama chetu, niliifuatilia mwanzo mwisho

Mbowe, hana tabia ya kuongea vile isipokuwa juzi katika kuwahutubia wananchi wa Mwanza na wanachama wa Chadema, sauti iliyotumika kuhutubia si ile tumeizoea,

Kwanza hotuba yake haikuwa na mpangilio, na mwenyewe pindi atakapoirejelea kuisikiliza, hatakubali tena kupanda jukwaani akiwa amelewa.

Naamini yako maneno mengi tu ambayo aliyatumia kusemea jinsi maridhiano yalivyokuwa, yaliashilia kuwa, Mbowe alikuwa tungi, baba mzima na heshima zake hawezi kutumia neno demu, eti maridhiano yalikuwa magumu kiasi cha mfano wa kutongoza demu? Huyu siyo Mbowe, bali ni pombe na Mbowe!

Kwa namna hii, washauri wa Mbowe, mmushauri aache kutumia kilevi kabla ya kuhutubia kwani atakuja kutukuna mitusi hiyooo! Tutaficha wapi uso wetu.
 
Mbowe ni kiongozi wangu,ila ukweli lazima usemwe alitukosea sana juzi kupanda jukwaani akiwa ameutwika. Hata mambo ya maana aliyozungumza watu wanayachukulia kuwa ni pombe tu.
 
Ulivyokuwa popoma, mshenzi na takataka unadhani hatuna smartphone za kuingia YouTube MATAGA sijui mnafeli wapi
Mitusi yote hii mkuu ni kwa sababu tu Mbowe alikunywa pombe?
 
Back
Top Bottom