Elections 2010 Mbowe atikisa mjini Arusha...


Nia ya kuibwaga CCM tunayo, sababu za kuibwaga tunazo na uwezo wa kuibwaga tunao. Shime watanzania halisi tukapige kura tarehe 31.10.2010.
 
huu muda mnaoutumia kudanganya watu ndio utakaowacost chadema, hamna kitu kama hicho hapa arusha!

Nime danganya nini lets be fair hapa mie sio CHADEMA kwa taaarifa yako sema siasa za wazi acha ushabiki ulikuwepo uwanjani NMC au nawe ni wa kuletewa habali na kujifanya wajua kuzi chakachua???

 
Baada ya mkutano wa Chadema kumalizika watu walijikusanya makundi makundi yaani Mianzini, garenaro,majengo nk na kuondoka huku wakishangilia na kungwa mkono watu mbalimbali hali hiyo iliwafanya polisi kutawanyika mji mzima wakiwa na mabomo ya machozi lakini nilijaribu kuzunguka sikuona wakitumia nguvu tofauti na week iliyopita pale polisi walipo tumia nguvu na kuvunja vioo, kupinga watu walio kuwa kwenye magari wakimsindikiza Bw Godbless Lema lakini leo nimeshuhudia wanachadema wakishangilia kwa makudi kama vile Taifa stars imeifunga brazil na hii ilimefanyika mbele ya polisi, CHADEMA walionyesha m'kali wa ajabu walikuwa wakipiga miluzi, mayowe, huku wakisema ni saa ya mabadiliko polisi kalaleni hakuna anaefanya fujo, wangine wakisema pipoooooooooooz, Kwa takribani dakika 30 barabara za Arusha mjini zilikuwa hazipitiki kitu kilichowafanya watu kusiamamisha magari ili wanachadema hao wajinafsi, nilipofika maeneo ya Sheikh Amri Abed Stadium, Blue rock, Golden Rose nilikuta umati mkubwa sana wa watu na magari matatu ya polisi wakiwa wamesima pembeni ya barabara kuwatazama CHADEMA, kuna kiongozi alikuja kuwaomba wasambae wasije wakasabaisha polisi wakatumia nguvu watu wa kaitika sawa kamanda nikaona kila moja akiondoka...lakini mimi nilijiuliza Kama Lema alikamatwa kwa sababu ya msafara wa zadi ya magari 30 wakaita maandamano iweje leo Mbowe haja kamatwa au wamesha anza kusoma nyakati
 
Hii ni people powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
kuna mwamko wa ajabu, hivi vitu nilishazoea kuviona siku ya Simba na Yanga...
 
nilifika mkutanoni mwisho mwisho kwenye saa kumi na mbili na nusu hv, watu walikuwa wengi sana, sio siri nilipata faraja mno. Mbowe alitangaza kuwa tar.30 ni mkesha wa kusheherekea uhuru wa pili tanzania.
 
Zito au dr slaa lazima arudi mwanza, busanda na tarime, kwimba kwa reticia nyerere hayo ni majimbo yanayohitaji final touch kuyaweka kibindoni

Mkubwa usemacho ni kweli. Na kama umechunguza kila slaa apitapo jk naye anarudi kule. Hivyo wakigawana mbowe tarime, zitto busanda, dk. Slaa mwanza watakuwa wamepiga bao. Ni mihumu sana kurudi for final touch.
 

All foam, no beer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…