BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mbowe awasha moto Mbeya
Ataka wananchi kuiga mfano wa Tarime
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi kwa sasa imesababishwa na mipango mibovu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mwenyekiti huyo alisema wakati umefika kwa Watanzania, hususan wananchi wa Mbeya Vijijini, kujiletea ukombozi kama walivyofanya wananchi wa Jimbo la Tarime kuachana na CCM.
Mbowe alisema hayo juzi wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbalizi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika baada ya mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho ulioidhinisha jina la Shitambala, kugombea ubunge Mbeya Vijijini.
Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho pamoja na wabunge wake, alisema nchi inayumba na hali ya maisha ya wananchi imezidi kuwa ngumu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kunakosababishwa na serikali ya CCM kushindwa kuweka mipango mizuri ya kuimarisha uchumi wa nchi.
Naomba niwaulize swali, hivi katika kipindi cha uongozi wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kipindi cha Benjamin Mkapa, kipindi kipi hali ya maisha ilikuwa na nafuu? Wananchi walijibu wakati wa Mwinyi, na Je, kipindi cha Mkapa na kipindi hiki cha Rais Jakaya Kikwete, kipi afadhali? Wananchi walijibu kipindi cha Mkapa.
Sasa kwanini mnaendelea kuikumbatia CCM, igeni mfano wa wananchi wa Tarime, alisema Mbowe.
Mbowe alisema ugumu wa maisha unaowakabili wananchi ni fundisho kwamba wasiendelee kuingangania CCM ambayo kimsingi haina mpango wa kuwaletea maendeleo na badala yake viongozi wa chama hicho wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kujilimbikizia mali.
Alisisitiza kuwa wananchi wa Mbeya Vijijini, wawaige wenzao wa Tarime ambao baada ya kunyanyaswa kwa muda mrefu na serikali ya CCM, wameamua kufanya mabadiliko ya viongozi, akiwemo mbunge ambaye anatoka CHADEMA.
Inashangaza kuona Mkoa wa Mbeya ambao una wananchi wengi wenye uelewa mkubwa lakini hakuna hata mbunge mmoja anayetoka chama cha upinzani, wakati ipo mikoa ambayo wananchi wake sasa wameamua kubadilika kwa kuwachagua wabunge kutoka vyama vya upinzani, alisema Mbowe.
Aliongeza kuwa hakuna mwananchi asiyefahamu kwamba wabunge wa CHADEMA wamefanya kazi nzuri bungeni ya kutetea masilahi ya nchi ambapo wamewezesha kuwafichua mafisadi walioanza kujilimbikizia mali, huku Watanzania wakiendelea kuwa maskini.
Alisema chama chake kitamsimamisha mgombea wake Shitambala katika Jimbo la Mbeya Vijijini ili kutoa fursa kwa wananchi wa jimbo hilo kupata mbunge kutoka chama hicho kama walivyofanya wenzao wa Tarime.
Alisema baada ya Kamati Kuu (CC), kupitisha jina la mgombea ubunge, viongozi waandamizi wa chama hicho wataweka kambi katika jimbo hilo kuhakikisha mgombea wao anachaguliwa.
Wakizungumza na Tanzania Daima, baadhi ya wananchi waliokuwepo katika mkutano, walisema wamechoshwa na serikali ya CCM na hawafikirii kukipigia kura chama hicho katika uchaguzi huo na uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Walisema Jimbo la Mbeya Vijijini ambalo wananchi wake ni wakulima, linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa pembejeo za kilimo kama vile mbolea, lakini serikali ya CCM imeshindwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Mbowe baada ya kumaliza kuhutubia mkutano huo pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, walirejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupanga mikakati ya kampeni za uchaguzi wa jimbo hilo, zinazotarajiwa kuanza Desemba 28 mwaka huu.
Jimbo la Mbeya Vijijini liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, marehemu Richard Nyaulawa, kufariki dunia Novemba 9, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Januari 25, mwaka huu.