Elections 2010 Mbowe awekewa pingamizi kugombea Hai

Hizo ni habari za Biashara!! Kama hotel ina deni, si inapigwa mnada?? Haya yamekujaje?? Ila kwa taarifa za kuaminika hili pingamizi limeshajibiwa na kupigwa chini. Mbowe ni mgombea halali wa ubunge kupitia Chadema! Soma gazeti la Mwananchi Augost 22, jana kuna majibu ya NEC front page "NEC yatupa pingamizi la Mbowe, Kingwangala".
 
 


Umesoma magazetini arafu unasema BREAKING NEWS??
 
Jamani tumsamehe bure labda hakujua maana ya neno 'abandoned'. Pole LeopoldByongje siku nyingine uwe unatembea na dictionary.
 
hii si breaking news kaka, ila hawa sisiemu mwaka huu hashindani na vyama pinzani kwa sera ila kwa kuweka pingamizi, kweli mwaka huu CCMmaji yako shingoni.CHADEMA oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
.....ningrshangaa kama NEC wangeiadmit hii appeal................!
 
Pingamizi alilowekewa limeonekana halina ushahidi na hivyo kutupwa toka majuzi (nadhani) huko jimboni
 
Mapingamizi mengine ni yakipumbavu. Hivi hao wanaokaa mpaka wanaingiza ishu za TRA kwenye moja ya kuwa sababu za mapingamizi wana akili kweli? Wameachwa mafisadi walioiba na kutumia madaraka vibaya. Ama kweli vioja mwaka huu tutaviona
 
Sheria inasema ukiwa umeshatiwa "hatiani",Haya malalamiko yalikuwa hayana nguvu.Kwasababu Kimbita ameshakuwa mbunge kwa miaka mitano lazima ana akili timamu, ninachukulia madhumuni ya malalamiko yake ni kumchafulia Mbowe jina, kutaka kuonyesha ni fisadi.

Hii habari sio breaking news ipo hapa toka jana kama sio juzi.
 
CCM wanajua upepo ni mbaya mwaka huu ndo maana wanatafuta kila mbinu kuokoa maisha yao,
Na ni dhahili kabisa wanashirikiana na msimamizi wa uchaguzi kuwahujumu wagombea wa vyama vingine, tumemwona Lawrence Masha alivyo abuse ofisi yake kwa kutumia wizara yake kumwondoa mpinzani wake wa chadema kwenye jimbo la nyamagana kisa eti sio raia wa Tanzania! hii ni aibu kubwa kwa nchi kuona mtu anatumia madaraka yake ya uwaziri wa mambo ya ndani kupika jungu na kuondoa ushindani ili apate mteremko, wanasheria wa chadema wako wapi? Tundu Lissu na Mabere Marando inabidi kumsaidia dogo wa chadema pale Mwanza ambaye ameeunguliwa kwani baba yake ni mtanzania na amezaliwa Tanzania, na dogo kazaliwa bongo kasomea bongo isipokuwa mama yake ndo mkenya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…