Pre GE2025 Mbowe: CHADEMA ni kubwa kuliko mtu yeyote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na clouds amesema
"Hapa Dar es Salaam kila Mtaa unaouona una uongozi wa CHADEMA wa Baraza la Chama, la viongozi wa chama.

Na katika Vijijini zaidi ya 12,000 zaidi ya 80% tuna viongozi katika vijiji nchi nzima na hatimaye sasa Vitongoji.

"Kuna Vitongoji 63, 000 nchi nzima tuna viongozi katika Vitongoji zaidi ya 50,000 nchi nzima.

"Ni mtandao mkubwa sana. Na ndio sababu wakati wote napenda kuwaambia Watanzania na hata viongozi wenzangu hiki Chama kimejengwa kwa nguvu kwa jasho na chama ni kikubwa kuliko Kiongozi yoyote ndani ya Chama hiki.

"Na Chama hiki ni kikubwa kuliko yoyote miongoni mwetu kama mtu binafsi. Ni taasisi kubwa, watu inayovuta na kuunganisha makundi mapana na makubwa sana"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Taratibu naanza kumwelewa........wacha niendeelee kumsikiliza, inawezekana kabisa Kwa wakati huu Mbowe anafaa kuendelea na nafasi anayo igombea.......tuendelee kumsikiliza.
 
Upuuzi tupu.

Ukiwa mkweli na Wala siyo mtu mnafiki, lazima utakubaliana na Ukweli mchungu Sana kwamba, Mbowe amepoteza mvuto wa kisiasa hapa Tanzania na duniani kote kwa ujumla wake. Mbowe amepoteza mvuto na ushawishi wa kisiasa, kimsingi amekuwa mtu ambaye hawezi kuaminika tena. Ni Mamluki na Ndumilakuwili. Ni hatari kubwa sana kwenye jamii ya Watu Kama chama cha siasa kuwa na mtu mwenye sifa mbaya za namna hiyo, anapaswa kuogopwa Kama kifo.
 
Anasema atahukumiwa kwa kukijenga chama na kukikuza.
Kwa sasa hakuna mtu mwwngine wa kukiendeleza chama zaidi yake.
Aachiwe miaka yake 5 hadi 2030 akamilishe aliyo yapanga.
 
Ukimsikiliza vizuri ni wazi kabisa katumia muda mwingi kukijenga chama na kukifikisha hapo kilipofika, asibezwe wala kuvunjiwa heshima.
 
CHADEMA hakuijenga yeye peke yake, Chadema imejengwa na Watu wengine wengi Sana, wakiwamo wanachama, wananchi wa kawaida wapenda Haki na mabadiliko ya kweli, na wanaharakati mbalimbali, n.k.
Watu wamejitolea gharama kubwa sana ya MACHOZI, JASHO na DAMU katika kuijenga CHADEMA. Alfonce Mawazo ameuawa kutokana na kuitetea Chadema, Tundu Lisu amemwaga DAMU yake nyingi Sana kwa ajili ya CHADEMA. Takribani 80% ya DAMU yote kabisa aliyonayo Tundu Lisu leo hii ni damu mpya kabisa aliyoongezewa baada ya kupoteza damu yake ya awali aliyozaliwa nayo katika harakati za kuitetea Chadema. Mbowe anapaswa kupisha wenzake ili waiongoze Chadema.
 
Kwann hajaandaaa mrithi mapema?
Kwann kila anayetaka kushindana naye kwenye sanduku la kura anajaa upepo na kupaniki?
 
Upuuzi tupu.

Ukiwa mkweli na Wala siyo mtu mnafiki, lazima utakubaliana na Ukweli mchungu Sana kwamba, Mbowe amepoteza mvuto wa kisiasa hapa Tanzania na duniani kote kwa ujumla wake. Mbowe amepoteza mvuto na ushawishi wa kisiasa, kimsingi amekuwa mtu ambaye hawezi kuaminika tena. Ni Mamluki na Ndumilakuwili. Ni hatari kubwa sana kwenye jamii ya Watu Kama chama cha siasa kuwa na mtu mwenye sifa mbaya za namna hiyo, anapaswa kuogopwa Kama kifo.
Yote hayo umesimuliwa! 😂😂😂
 
Taratibu naanza kumwelewa........wacha niendeelee kumsikiliza, inawezekana kabisa Kwa wakati huu Mbowe anafaa kuendelea na nafasi anayo igombea.......tuendelee kumsikiliza.
Kanadi sera ipi?

Hakuna watoto, sisi wote ni watu wazima. Ijapokuwa itasemwa ukweli halisi haujulukani lakini Mungu ametupatia uwezo wa kuunganisha.

Kwamba hapa kuni anaziwasha huyu anataka kutengeneza moto! Anachukua unga tena dona anauweka kwenye sufuria na kuinjika kwenye moto!! Hapa huyu anataka kutengeneza ugali!

Anakata mboga mboga za majani! Hapa anatengeneza mboga.

Mbowe yote anayozungumza naona ni upuuzi sioni chochote cha maana anachokizungumza.

Hana sera, na yeye anajua hana sera! Anachokifanya kwa sasa anatafuta huruma.

Tukiitafuta logic pasipo kuingiza hisia za namna yoyote imma ziwe za kisiasa au kidini au za kikanda na tukiangalia hali halisi ya namna jinsi ilivyo kwa haya yanayozungumzwa, Mbowe inambidi akae pembeni.
 
Mwenyekiti wa CHAFEMA Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na clouds amesema
"Hapa Dar es Salaam kila Mtaa unaouona una uongozi wa CHADEMA wa Baraza la Chama, la viongozi wa chama.

Na katika Vijijini zaidi ya 12,000 zaidi ya 80% tuna viongozi katika vijiji nchi nzima na hatimaye sasa Vitongoji.

"Kuna Vitongoji 63, 000 nchi nzima tuna viongozi katika Vitongoji zaidi ya 50,000 nchi nzima.

"Ni mtandao mkubwa sana. Na ndio sababu wakati wote napenda kuwaambia Watanzania na hata viongozi wenzangu hiki Chama kimejengwa kwa nguvu kwa jasho na chama ni kikubwa kuliko Kiongozi yoyote ndani ya Chama hiki.

"Na Chama hiki ni kikubwa kuliko yoyote miongoni mwetu kama mtu binafsi. Ni taasisi kubwa, watu inayovuta na kuunganisha makundi mapana na makubwa sana"- Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA
Huu ndio ukweli wa mambo.
 
Upuuzi tupu.

Ukiwa mkweli na Wala siyo mtu mnafiki, lazima utakubaliana na Ukweli mchungu Sana kwamba, Mbowe amepoteza mvuto wa kisiasa hapa Tanzania na duniani kote kwa ujumla wake. Mbowe amepoteza mvuto na ushawishi wa kisiasa, kimsingi amekuwa mtu ambaye hawezi kuaminika tena. Ni Mamluki na Ndumilakuwili. Ni hatari kubwa sana kwenye jamii ya Watu Kama chama cha siasa kuwa na mtu mwenye sifa mbaya za namna hiyo, anapaswa kuogopwa Kama kifo.
Hata Saa100 amepoteza mvuto sana,ila hakuna namna
 
Ukimsikiliza vizuri ni wazi kabisa katumia muda mwingi kukijenga chama na kukifikisha hapo kilipofika, asibezwe wala kuvunjiwa heshima.
Haimpi mandate ya kuona kwamba mtu mwingine akigombea ni usaliti
 
Anasema atahukumiwa kwa kukijenga chama na kukikuza.
Kwa sasa hakuna mtu mwwngine wa kukiendeleza chama zaidi yake.
Aachiwe miaka yake 5 hadi 2030 akamilishe aliyo yapanga.
We jamaa vipi wewe, amekaa kwenye kiti zaido ya miaka 20 na hajakamilisha hayo mambo. Je unajua ni yapi anayotaka kukamilisha?
 
Back
Top Bottom