Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wakati Trump anaibuka kugombea urais mwaka 2016 alipingwa karibia na establishment yote ya chama cha Republicans, alikuwa anaonekana mropokaji na kituko tu mbele ya "wenye chama", hakuna aliyedhani angefika mbali ila leo hii ni Rais wa Marekani kwa awamu ya pili.
Kama wajumbe tu wa chama cha Republicans ndio wangekuwa wanapiga kura kwa uhakika Trump asingetoboa, angeshindwa vibaya sana, bahati yake nzuri wanachama wote ndio waliokuwa wapiga kura kumchagua mgombea Urais.
Sasa hivi Trump ile Republican ya zamani yote kaifagilia mbali, kama wewe sio movement yake ya MAGA huwezi tuna kufurukuta au kusikika ndani ya chama cha Republicans. Miamba ya Republicans wakina Familia ya Bush, Dick Cheney, John Bolton, John Boehner, Paul Ryan na wengine wengi waliomkataa Trump wamepotea kabisa katika siasa za Republicans na nchi ya Marekani.
Kwa upepo uliopo ninaamini kama kura zingekuwa zinapigwa na wanachama wote wa CHADEMA Mbowe hawezi kushinda ila kwa wajumbe wa CHADEMA anaweza kushinda kwa sababu zozote zile(sio jambo la ajabu wajumbe wengi kuwa disconnected na uhalisia uliopo kwa wanachama wao na raia kwa ujumla)
Mbowe itakusaidia nini ukishinda kwa wajumbe halafu wanachama na raia hawako pamoja na wewe? Utakuwa umeisaidiaje CHADEMA katika hali hiyo?