sonofobia
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 1,171
- 4,295
Kijana Deus Soka umeipambania Chadema kwa jasho na damu. Mara kadhaa umekaa jela, umepigwa, umeumizwa umepitia madhila mengi ukiamini unapigania mabadiliko ya kweli.
Ulikuwa mstari wa mbele kuipigania katiba mpya tulikuona ukipigwa virungu na mateke ulipojitokeza na wenzio kumi maandamano ya kupinga mkataba wa DP world.
Ulifanya mengi ukiamini upo chadema sehemu sahihi ya kuitafuta haki.
Lakini leo haupo, Mbowe anasifia uongozi wa Samia. Kwenye speech yake ya kutangaza kugombea uenyekiti hakuna sehemu amezungumzia wewe na wenzako mliopotea yeye anasema kuhusu mafanikio ya Samia.
Tumeona machawa wa Mbowe walikubeza wakisema umejiteka yote sababu wanajua ulitaka kugombea uenyekiti bavicha taifa utu umewatoka kisa nafasi ya kisiasa mpaka wanasema umejiteka. Pengine kuwa karibu na mentor wako Lissu ndio maana hawajali kuhusu wewe.
Naamini uko ulipo ni mzima na utarudi salama, yoyote aliyekuchomesha atalipa.
Mbowe atalipa machozi ya vijana kama Soka waliomini wanakufa na kupotea sababu ya chama kumbe wamekuwa wakitumika leo anasema hizi siasa zimepitwa na wakati siasa za kisasa ni kukaa mezani na kugawana kibuyu cha asali.
Mbowe utalipa machozi ya Soka inshaAllah.