Mbowe hata akishinda atakuwa kama ameshindwa tu.

Mbowe hata akishinda atakuwa kama ameshindwa tu.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Bila shaka umewahi sikia kuhusu msemo Pyrrhic Victory. Msemo huo unamaanisha ushindi uliopatikana kwa gharama kubwa kiasi kwamba umekuwa sawa na kushindwa. Miaka kama 300 kabla ya Yesu mfalme mmoja wa ufalme mdogo wa Kigiriki aliyeitwa Pyrrhus alipigana na Waroma. Alishinda vita ila alipoteza watu na mali nyingi sana kiasi kwamba ikawa kama ameshindwa.

Mbowe hata akishinda na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti ushindi wake utakuwa ni kama ule wa Pyrrhus. Atapoteza vitu vingi sana kwake binafsi na kwa chama. Kwanza kelele za kuwa anang'ang'ania madaraka ndiyo zitazidi. Heshimu yake itashuka na kuwa kama wakina Lipumba, Mrema na wang'ang'ania madaraka wengine. Hii ni hasara kubwa kwa mtu anayeheshimika kama Mbowe. Pili, hili linategemea hatua atakayochukua Lissu baada ya kushindwa ila ni kama chama kitampoteza Lissu na wanaomuunga mkono(Wanachama wengi sana). Wanaweza kuamua tu kuwa baridi. Tatu ni kuwa imani ya watu kwa CDM kama chama kinachopaswa kupewa madaraka otashuka sana.

Njia pekee ya Mbowe kushinda ni kutogombea.
 
Back
Top Bottom