Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema miaka saba iliyopita ilikuwa ya bonde la maumivu makali kwa wananchi wote. Alitaja maumivu hayo akihusisha wale waliofungwa magerezani na watumishi waliofukuzwa kwa kigezo cha vyeti feki.
Mbowe aliyasema hayo jana mkoani Njombe alipokuwa akiwahutubia wananchi mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya hadhara baada ya kuruhusiwa hivi karibuni.
“Wako walionyang’anywa mali, Tanzania ikageuzwa kuwa Taifa la mateso, wananchi wakaishi kwenye hofu, lakini kwa wiki moja tuliyofanya mikutano ya hadhara, nikiliangalia Jeshi la Polisi silielewi mbona limekuwa na ubinadamu hivyo,”alisema Mbowe.
Alisema miaka saba iliyopita jeshi hilo halikuwa hivyo, lakini wanashukuru kwa sasa hali hiyo imebadilika na wanaamini kiongozi wa nchi anatengeneza vyombo vya dola kwa kuzingatia misingi ya kujali haki kwa wote.
“Tunachokiona leo ni Tanzania tunayoipenda Chadema tukizungumza, polisi wapo wanalinda amani na wanasikiliza sera.Tulifika hatua polisi wetu walionekana maadui kwa wananchi na raia, walikuwa wanawaombea mambo mabaya,”alisema.
Kiongozi huyo alisema vyombo vya ulinzi na usalama siku zote vinapaswa kusimamia amani, huku akieleza siku chama hicho kikishika dola hawataagiza polisi kutoka mataifa mengine, bali vijana hao wataendelea na wajibu huo katika mazingira bora.
“Msipendelee Chadema, simamieni haki kwa vyama vyote, thawabu yenu mtaipata duniani na mbinguni lakini mkipewa amri za kuhatarisha amani, msizisikilize,”alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa alisema sera ya chama hicho imekuwa ikizungumzia sera ya majimbo, inayosisitiza watu katika maeneo yao wawachague watu wenye uwezo wa kuwawajibisha wale waliowachagua pale wanapobaini uwezo wao ni mdogo.
Kilimo
Akizungumza suala la kilimo, Msigwa alisema katika maeneo mbalimbali waliyozunguka kipindi hiki cha mikutano, wakulima wa mazao mbalimbali yakiwamo ndizi, parachichi, kahawa, cocoa, pareto, mpunga, mahindi, bado wanatekeleza kilimo chao kwa gharama kubwa.
“Na mazao mengi yanalimwa kanda ya Nyasa, halafu anakuja mtu mmoja ambaye hajulikani anakuja kuwapangia namna ya kutumia rasilimali zenu hili haliwezekani,”alisema Msigwa.
Alinukuu maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa aliwaambia wananchi wa Njombe, ili waweze kuendelea wanahitaji vitu vitatu ambavyo ni watu, ardhi na siasa safi.
Credit: MWANANCHI NEWSPAPER