Elections 2015 Mbowe kabadili gia angani, ndege inaanguka!

Elections 2015 Mbowe kabadili gia angani, ndege inaanguka!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Gazeti la Raia Mwema leo lina Makala nzuri sana ya kudadisi matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu.

Mbowe ali "m-procure" Lowassa dakika za mwisho kabisa katika kumpata mgombea wa urais baada ya Lowassa kukatwa nafasi hiyo huko CCM.

Wakati huo Mbowe akitamba kuwa amebadili gia angani, kitendo ambacho kimsingi hata kwenye ndege yenyewe hakiruhusiwi-maana ndege ni lazima itaanguka tu.

Mbaya Zaidi Lowassa mwenyewe aliingia UKAWA kwa gia moja tu, nayo ni kugombea urais, bila kutilia manani msimamo wa CHADEMA uliokibeba kwa miaka mingi, msimamo wa kupinga ufisadi.

Na Zaidi ya hapo msimamo huo wa kupinga ufisadi ulitokea dirishani, na haukuwa na mashiko katika kampeni.

La kuhuzunisha ni kuondoka kwa wapiganaji amhiri wa upinzani katika UKAWA, Dr Slaa na Prof Lipumba.

Ukijumlisha yote, kwa watu makini, uadilishaji huu wa gia angani umeleta matokeo yasiyo na tija kwa Upinzani , UKAWA na hata CHADEMA yenyewe.

Siyo siri, ndege ya CHADEMA inendelea kuelekea ardhini na kuanguka, matokeo yanajieleza.
 
Bado faida imeonekana ukawa....hakuna walichopoteza labda useme Lowassa kapoteza
 
jumbo jet limesha tua zanzibar linajaza mafuta litakuja bara mda siyo mrefu!
 
Ajabu ni kwamba wanaoijadili CHADEMA wao siyo CHADEMA, unashangaa CDM kuanguka, Shangaa Nchi kuanguka! Na mlivyotumia peas nyingi hivyo kwa uchaguzi Huu Naona jinsi Maisha yatakavyotuwia magumu Sana ndani ya miaka miwili Ijayo Chini ya utawala wa Mabavu. Na wala sitoshtuka kusikia Mmesaini mikataba kandamizi ili mfidie pesa mlizoteketeza ktk uchaguzi Huu!! Na wenye vyuo watapandisha ada maradufu!!! MIAFRICA NDIVYO TULIVYO!
 
Kama hujajua CDM wameongeza wajimbo mangapi bora ungeacha kuweka thread yako ya kidhaifu kama hii! Huna facts kabisaa, hujui kinachoendelea. CDM hadi sasa wameshaongeza majimbo 12 ukilinganisha na mwaka 2010, CUF sisemi unaona mwenyewe!
 
Bado faida imeonekana ukawa....hakuna walichopoteza labda useme Lowassa kapoteza

CHADEMA wamepoteza pia.Wanachama na wapenzi wao walichanga mabilioni Lowasa aende ikulu.Lengo kuu halikuwa kupata wabunge wengi wala madiwani wengi lengo kuu ilikuwa ikulu.

Wachangiaji CHADEMA huwezi kuwaambia sijui tumepata madiwani wangapi au sijui wabunge wangapi hawataki hata kusikia.Walitaka Lowasa AENDE IKULU.Na CHADEMA kilitaka hivyo.Hivyo kimepoteza pia.Lowasa kapoteza pesa zake naye bure.Ila mimi naona poa tu sisemi kapoteza bali kawarudishia wananchi sehemu ya pesa zao
 
Fisadi akiwa nyumba ya jirani, akija kwako mtakatifu!
Nyumbu atabaki kuwa nyumbu tu. Hataitwa ng'ombe hata siku moja
 
CHADEMA wamepoteza pia.Wanachama na wapenzi wao walichanga mabilioni Lowasa aende ikulu.Lengo kuu halikuwa kupata wabunge wengi wala madiwani wengi lengo kuu ilikuwa ikulu.

Wachangiaji CHADEMA huwezi kuwaambia sijui tumepata madiwani wangapi au sijui wabunge wangapi hawataki hata kusikia.Walitaka Lowasa AENDE IKULU.Na CHADEMA kilitaka hivyo.Hivyo kimepoteza pia.Lowasa kapoteza pesa zake naye bure.Ila mimi naona poa tu sisemi kapoteza bali kawarudishia wananchi sehemu ya pesa zao

Mkuu umenena!
Lowassa ndo kwishney
Mbowe anahaha kuonyesha mafanikio ya kumleta Lowassa kwa gia ya angani.
Alichopewa kitamsumbua sana.
 
Hivi magufuli na shein waneshinda eehee.!?
 
Gazeti la Raia Mwema leo lina Makala nzuri sana ya kudadisi matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu.

Mbowe ali "m-procure" Lowassa dakika za mwisho kabisa katika kumpata mgombea wa urais baada ya Lowassa kukatwa nafasi hiyo huko CCM.

Wakati huo Mbowe akitamba kuwa amebadili gia angani, kitendo ambacho kimsingi hata kwenye ndege yenyewe hakiruhusiwi-maana ndege ni lazima itaanguka tu.

Mbaya Zaidi Lowassa mwenyewe aliingia UKAWA kwa gia moja tu, nayo ni kugombea urais, bila kutilia manani msimamo wa CHADEMA uliokibeba kwa miaka mingi, msimamo wa kupinga ufisadi.

Na Zaidi ya hapo msimamo huo wa kupinga ufisadi ulitokea dirishani, na haukuwa na mashiko katika kampeni.

La kuhuzunisha ni kuondoka kwa wapiganaji amhiri wa upinzani katika UKAWA, Dr Slaa na Prof Lipumba.

Ukijumlisha yote, kwa watu makini, uadilishaji huu wa gia angani umeleta matokeo yasiyo na tija kwa Upinzani , UKAWA na hata CHADEMA yenyewe.

Siyo siri, ndege ya CHADEMA inendelea kuelekea ardhini na kuanguka, matokeo yanajieleza.

Mbona chadema imefanikiwa sana kuliko munavyo sema. Figisufigisu za ccm zinaelekea mwisho.
 
Gazeti la Raia Mwema haliuziki bila kuandika UKAWA.
Hakuna mtu anaye ingia kwenye uchaguzi akitaka kushindwa kila mtu wakati wa kampeni lazima ahubiri kushinda. Ukishindwa unafanya analysis unasonga mbele.
Kipindi chote cha kampeni nilikuwa Sukumaland yaani Geita, Simiyu na Mwanza. Kura nimepigia mkoa wa Mwanza. Huku KAMPENI haikuwa ya sera wala chama. SLOGANI ya huku ni CHAGUA MAGUFULI MSUKUMA MWENZETU basi. Mimi nilidhani ni kwa wananzengo peke yake.
Kwa Mwanza mjini hasa maeneo ya SAAWA, BULALE, KISHIRI, SANGABUYE na vijiji vingine pembezoni mwa jij ilikuwa TUCHAGUE WASUKUMA WENZETU WAGENI WAKAGOMBEE KWAO... kwa kweli hali ilikuwa hivyo kote.

Baaada ya matokeo kutoka marafiki zangu wengi sana tena wengine wana PHD wasukuma wa Mwanza wote wanaimba hivyo hivyo tu Mwanza kwa wasukuma tu. Kwa walioshinda wanaona ni strategy nzuri lakini najiuliza kama mwanza ni kwa akina bageshi peke yake basi wasukuma walioko mpanda, usangu, kilosa wote nao warudi mwanza?
 
we inakuuma nini chadema kupoteza au ndio mambo ya usengerema? kwanini usiijadili Chama Cha Majambazi yako yalioyoiba kura kila kona? Acha unafiki kujifanya unaijadili chadema kinafikinafiki

#NAICHUKIACCMTOKAMOYONI
 
Mbona chadema imefanikiwa sana kuliko munavyo sema. Figisufigisu za ccm zinaelekea mwisho.

Acha kujihadaa wewe! Kuna maeneo Ukawa imeshinda Diwani, Mbunge na Halmashauri lakin kwa Lowassa hapana wengine waliamua kumpa Magufuli na wenye chuki zaid na ccm wakaamua kuharibu Kura. Kiburi cha Lowassa haikuwa Mafuriko ya watu alijipa matumaini ya kuwatumia vijana wake waliokamatwa kwa kupika matokeo na kuyaingiza kwny mfumo rasmi wa mAtokeo kwa haramu za kimtandao. Dr.Slaa chini ya Ukawa angeleta mafanikio zaidi kuliko huyu Fisadi Mgonjwa.
 
Hivi wako wapi wale watabiri wetu wa kudumu akiwemo mshenga? Au wakfu wa utabiri sasa umesombwa na mafuriko ya li tinga tinga?
 
Bado faida imeonekana ukawa....hakuna walichopoteza labda useme Lowassa kapoteza

Ni kweli kwamba UKAWA wmenufaika na kubadilisha gia angani japo ndege imeanguka vibaya sana, chadema wamepata wabunge kwa kupitia mtaji wa Lowasa japo Lowasa mwenyewe kaingia hasara kubwa sana, hakupata alichokuwa akitafuta na sijui atafidiwa vipi na chadema.
 
Na mantiki yenyewe ni kuwaandaa watanzania kisaikolojia kuwa makuful atashnda ili kurahisisha bao la mkono..
Siyo bao la mkono kaka! Lowassa anapumulia mashine! Ile ya saa mbili asubuhi atakuwa ametangazwa mshindi ndiyo hamna tena. Na wale mamluki wa ICT kuja kuhack mtandao wa Tume ndiyo wapo segerea!
 
Shigongo aliwahi sema siku moja kuwa limbowe ni lijanja na hilo linadhihirika Leo amemtumia Lowasa kama jembe la kupalilia shamba lake la CDM ili avune ruzuku nene.
Pole Lowasa, Kingunge na mijitu mingine iliyotoswa kwe mtumbwi wa vibwengo, Mbowe take yataenda kama kawaida kila nyie mmeanguka vibayaaaa!
 
Back
Top Bottom