Uchaguzi 2020 Mbowe kabugi step?

Mbogo nyeusi

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
233
Reaction score
541
Nimeona humu Kuna kundi linampondea Freeman Mbowe kutangaza nia ya kugombea urais mwaka huu 2020,

Kwa maono yangu naona yupo sawa siyo kwa maana ya katiba ya nchi au chama,kwa vile mtangaza nia mkuu anaye tegemewa kwa Sasa hayupo nchini na inawezekana muda ukafika na ikashindikana kuingia nchini kutokana na kuhofia usalama wake,ikitokea hivyo maana yake chama kitakuwa hakijajiandaa kuwa na mtu imara,kwa hiyo kuwepo kwa watangaza nia Kama Freeman na Nyalandu ni maandalizi mazuri ya kufikia October,Nina imani kuwa siku lisu akiingia hapa nchini salama Mbowe atajitoa kiroho Safi,hofu ipo kwa Lisuuuuu atarejea na usalama wake utakuwaje?hawa wanaomnanga Mbowe humu ni hofu tu walifikiri chama kimekufa.
 
Mbowe ni pandikizi la CCM!
 
CDM wana strategy kali sana wee subiri utaona, unafikiri Mbowe anafanya mamboa bila akili? Yajayo mtafurahi.
 
CDM wana strategy kali sana wee subiri utaona, unafikiri Mbowe anafanya mamboa bila akili? Yajayo mtafurahi.
Khaaaaaa, yani unadai CHADEMA wana akili? Kweli DJ Gambe kawaweza
 
Kuna kipindi huwa nawaza hivi.

Binafsi sijawahi kuamini mfanyabiashara mkuu kuwa mwanasiasa mtetezi wa wanyonge.
Kila kitu ni kama lakini kubwa ni kuangalia unalijazaje tumbo na kulinda maslahi yako!
 
Khaaaaaa, yani unadai CHADEMA wana akili? Kweli DJ Gambe kawaweza
Wewe fikiri mtu mmoja tu, lakini majeshi yote ya ulinzi, polisi, bunge, usalama wa taifa, na kikundi kutoka chattle hawalali, kweli Mbowe komando.
 
Mbowe sio lazima awe yeye kuna watu pale kuna mnyika, kuna heche angalau ana shahada moja mbowe alitakiwa kuwa pembeni kabisa bora hata wamama wakina matiko, mdee au bulaya.
 
Wewe fikiri mtu mmoja tu, lakini majeshi yote ya ulinzi, polisi, bunge, usalama wa taifa, na kikundi kutoka chattle hawalali, kweli Mbowe komando.
Yaani bangi zinawaharibu sana, Mbowe angekuwa anatafutwa si angefyatuliwa kiuno tu dk 0.
 
Kwa sababu Kuna jembe zaidi yake

Lissu alikuwa wa kwanza kutangaza nia, lakini baada yake ikawa kila mmoja anaibuka... hili limemvunja moyo Lissu usitegemee atakuja.

Tulimpamba kuwa ni yeye pekee, ona sasa..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…