Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,864
- 5,695
Nimemsikiliza Mbowe kauli zake ktk hotuba aliyo itoa nafikiri sio yeye aliye iandika ametumika kama spika.Navyo mfahamu huko nyuma kariba yake jana nimewaza tofauti kabisa na nilivyo muheshimu japo bado namuheshimu.
Kwanza Mbowe anasema ameamua kugombea kwa kuwa hajaona mtu sahihi wa kuiongoza Chadema. Ina maana kwa miaka zaidi ya ishirini aliyoongoza Chadema hajaona mtu hata mmoja mwenye akili zaidi yake ni matusi. Kwahiyo hata wale viongozi wa kanda walio enda kumsindikiza na kumshauri anawaona ni manyumbu na mamburula hatari.
Najiuliza Mbowe ni mwanadamu akifa chama atakiacha kwa nani? Na akiwa amekufa ikatokea chadema kimepata kiongozi mbovu atafufuka kuja kuokoa jahazi?
Mbowe anadai maridhiano yameleta faida eti kununua jengo na walio kuwa ukimbizini kurejea. Mbowe anasahau hali ya usalama sasa ni mbaya kuliko wakati wa Magufuli. Watu wanatekwa na kuuawa mchana kweupee hadi sasa viongozi wa Chadema hawajulikani walipo. Ruzuku sio hisani pesa ya kisheria asidanganye watu Chadema ndio walikataa kuchukua.
Mbowe ajuwe kuwa sisi Chadema ndio tulio onesha imani dhidi yake wakati CCM wanamtukana na kumkejeli kuwa ni kilaza. Imani hiyo tuliyo mpa asifikirie anaimiliki cheo ni dhamana.
Mbowe amejidhirisha kuwa haaminiki kwa kauli zake. Uchaguzi ulio pita alisema amelazimishwa kugombea na ni muhura wake wa mwisho. Leo anasema anarudi mzigoni kugombea huyu sio mkweli na hizi sio sifa za kiongozi.
Pili anasema Magufuli alitaka kumuhonga akakataa. Kwa nini usubirie mtu mpaka afe ndio useme mabaya yake? Magufuli hawezi jitetea kwa kuwa yupo kaburini alipaswa aseme akiwa hai na muhusika asikie na kujitetea ikiwezekana.
Kama ni kweli uliahidiwa na ukakaa kimya inamaana Mbowe anashiriki na kubariki vitendo vya rushwa na madili, Ilikuwa ni wajibu wake kutoa taarifa ili vyombo vinavyo husika vichukue hatua hta visipo chukua hatua basi kumbukumbu itakuwepo. Tutaamini vipi sasa hivi kuwa hamkukubaliana?
Jambo jingine la kuudhi ktk hotuba ya Mbowe ni kwamba anaifanya Chadema kama miliki yake. Anaipangia lini yeye ataongoza mpka akistaafu kwa umri huo basi Chadema itakuwa na kiongozi mpya. Viongozi Chadema hupatikana kwa kura wala sio hisani hii ni taasisi.
Wajumbe mtakao kwenda kuchagua Viongozi mnao wajibu mkubwa wa kujua ni wakati huu wanachadema na wananchi wanahitaji.
Watanganyika wanataka madiliko. Wasipo yapata ndani ya Chadema hawata kata tamaa watayatafuta nje ya Chadema. Ni wajibu wenu kufanya maamuzi kwa misingi ya kitaasisi au kufanya maamuzi ya kumchagua Mbowe aendelee kutuita sisi wanachadema ni manyumbu ndio maana ameamua agombee tena kwa kuwa hajaona mtu sahihi.
Maendeleo hayana vyamaa.