KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
MBOWE KATAA MTEGO HUU WA KUOMBWA KUENDELEA KUWA MWENYEKITI.
Mwl. Nyerere kila alipotaka kung'atuka wapambe waliandamana kumtaka aendelee wakimwambia Nchi hii changa bila wewe tutakwama, Bila wewe hatuwezi kwenda popote na Mwl. aliwasikiliza akawakubalia lkn mwishoni aliamua kufanya maamuzi magumu akang'atuka na ndipo alipogundua waliokuwa wanampanga hawakufanya hivyo kwa maslahi ya Nchi bali ni kwa maslahi ya matumbo yao na familia zao.
Mbowe linda heshima yako uliyoijenga kwa miaka mingi kwa jasho, machozi, damu na fedha kwa kuwakataa hao wapambe na wito wao.
Kama kweli wanakupenda mbona ulipoitisha maandamano hawakutoka kwa idadi kubwa kama ile kukusapoti??
Kwenye maandamano hawatoki kukusapoti ila kwenye kugombea ndio wanafurika kukutaka ugombee huwezi kujiuliza hawa ni watu wa aina gani???
Mbowe wasikilize familia yako na wenye mapenzi mema na wewe pumzika kwa heshima waachie wengine waendelee ulipoishia baki na heshima yako katika mageuzi kwani utake usitake kuna siku utatoka tu hapo.
Wahuni wengi na wanufaika wa mfumo uliopo ndio huwa na mashaka na mabadiliko ya uongozi lkn kila mabadiliko yalipotokea mambo yaliendelea kama kawaida.
Hata baada ya kifo cha Magufuli kuna watu waliamini mambo yangesimama lakini wote ni mashahidi mambo yanasonga mbele.
Mbowe dhihirisha kuwa chama chako ni cha kidemokrasia, dhihirisha kuwa wewe sio muumini wa kung'ang'ania madaraka, dhihirisha kuwa wewe ni mtu unayesoma nyakati na mazingira katika uongozi. Pumzika kwa heshima yako na historia itakukumbuka kama mwamba wa siasa za mageuzi Nchini.