Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
“Huu uliofanyika ni ukandamizaji ambao sio wa kawaida na wala usionekane ni tukio dogo, sisi kama Chama tunachukua jambo hili kwa uzito mkubwa sana na tunaamini jambo hili ni mkakati wa makusudi uliotengenezwa na Serikali, Vyombo vya vya Ulinzi na Usalama likiwemo Jeshi la Polisi, CHADEMA hakijawahi kuwa Chama cha kigaidi, shutuma za Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa ni baseless na reaction ya Polisi ni baseless”
“Chanzo cha yote haya kisingizio kilichopelekea Watu kuumizwa, ni kodi zenu, hii oparesheni ime-cost Jeshi la Polisi Mamilioni ya kodi za Walipakodi wa Nchi hii kwa Watu kulipwa posho n.k, hivi kweli pesa zetu zinapaswa kutumika kwa mambo ya kihuni!?”
“Serikali ina hofu inasema tunaweza kuleta machafuko kama ya Gen Z wa Kenya napenda kuiambia Serikali yaliyotokea Kenya na ambayo yametokea kidogo Ghana, yametokea Nigeria, Uganda, hii presha itakua na itaongezeka, wala huku kupiga Viongozi sio suluhisho, Kenya walipuuzia malalamiko ya Gen Z, Serikali ya Kenya ilipuuza kilio na maumivu ya Wananachi, Wananchi wakafika mahali wakachukua hatua, tunawaambia Tanzania haitokuwa tofauti kama CCM haitobadilika, hilo walielewe sio mabomu, sio vifo, tunataka wawasikilize Wananchi”
“Wakishupaza shingo wakifikiri kurejesha mitutu barabarani itazuia movement wanajidanganya, Serikali ya Tanzania ijifunze, wahangaike kujua wanajikwaa wapi, wasihangaike na CHADEMA, uhuni uliofanyika uchaguzi wa 2019 na 2020 kama ndio wanakusudia kuufanya 2024 na 2025 tumewaonya mapema sana, hii Nchi haitokuwa salama”
“Wajifunze kwa namna tukio la siku 3 tu limevuta Global attention, Vyombo vya Habari vya Dunia nzima vinaripoti kuhusu Tanzania, tukikaa kimya ndani Dunia itasema, narudia Chama chetu sio Chama cha kigaidi “ —— Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - CHADEMA: Tutafungua kesi dhidi ya Sisty Nyahoza na Awadh Haji juu ya kukamatwa na kupigwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA