Elections 2010 Mbowe, Marando, Slaa, Zitto, Lissu, Mnyika

This is a very thorny situation; Wabunge wanataka watimize wajibu wao waliotumwa na wapiga kura wao. Lakini ata the same time ili kukamilisha majukumu yao, wanatakiwa wakaribishwe na matu wanayeamini kuwa hastahili kuwakaribisha bungeni. Je wakimfukuza au kumkataa, ni nani atakayewakiribisha kufanya shughuli walizotumwa?

Ninadhani kuwa jambo mojawapo wanaloweza kufanya ni kuwepo Bungeni ila watafute utaratibu mzuri wa kufikisha ujumbe wao kuwa hawamtambui Kikwete kama rais halali wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kuyapata madaraka hayo kwa njia dubious, ila watamsikiliza kwa katika kikao kile kwa vile sasa hivi nchi haina rais halali kutokana na yeye kukamata madaraka hayo.
 
kama posho si issue kubwa kwa chadema, tunaomba ile ahadi ya elimu bure ianze sasa kwa michango ya wabunge wenu kusomesha angalau watoto mayatima ktk majimbo yao ndipo kauli ya posho sio issue iwe ni kweli!!!

POINTLESS Mkuu hii umetoa; du hivi pia ni mtu mzima au mtoto so tukusamehe?
 
Habari za uhakika Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh. Said Arfi ametetea kiti chake cha ubunge Mpanda Mjini. Safu imekamilika sasa ni kujipanga kwa kwenda mbele keep it up Chadema.
 


upo sawa mkulu
 

Kamanda, hoja ya kisaikolojia matters so much. Scan media uone kwa nini only 42% ya wapiga kura walijitokeza. You will be amazed jinsi propaganda ilivyofanya kazi na vitisho kuscare watu wasije. Take it or leave it, our life and what we do depends so much on your own pyscholgy, attitude and perception which is what I am talking about.

More than 3 times Dr. Slaa amewaomba Watanzania wawe na subira wakati wanalifanyia kazi na kutafakari jinsi ya kutoa official statement and stand juu ya matokeo. Now why rush now kususia hotuba wakati hata sababu zote za kukataa matokeo bado hazijawekwa wazi officially kama Dr. Slaa na CHADEMA wanavyosema. Kama wangekuwa wameshatoa evidences, inge-make a lot of senses bila kuzua potential mtafaruki.

(Sorry, too much of Kiswanglish . . . . Ni kwa sababu mama Koku, hajanipa breakfast ya supu ya kuku niliyoagiza kutoka USA ambako daughter wangu yuko Havard University anasoma. Alikwenda na Gulf Stream ya JK.)
 

Dr.Slaa

Nakubaliana na wewe kabisa.
Tuko nyuma yako na tunaomba kweli msikurupuke. Hotuba ya JK tunaomba muitose kwa kutoka nje ili kuonyesha kuwa haki haikutendeka kwenye Uchaguzi wa Urais na Ubunge wa 2010. Baada ya Speech ambayo I beliewe won't take more than 2 hours mtarudi mjengoni kuendelea na taratibu zingine.

Tunataka JK aelewe kuwa ana-deal na watu waliokwenda shule wasiobabaika na wanaosimamia sheria,haki na demokrasia ya kweli.


Thanks
 
haihitaji kutafakari sana...CHADEMA MPs nyanyukenikwenye viti vyenu na mtoke nje mara tu JK anatakapoanza kuhutubia bunge...Mbona wamarekani UN walitoka nje mara Gadafi alipoanza kuhutubia na kuirarua katiba ya UN???acheni uwoga bana ..
R u serious? sidhani kama ni wazo zuri sana. Na dhani ni vyema wakasikiliza ili waweze kutoa hoja zao. Wakifanya hivyo inaweza leta tafsiri ambayo si nzuri. Ni mawazo tu, sory!:bowl:
 
Kama chadema haitambuwi matokeo ya nec yaliomtangaza kikwete kama mshindi basi hawana haja ya kusikiliza hotuba ya Kikwete.

Naona watu wanatoa comments kwamba wabunge wa chadema wakitoka kwenye ukumbini wakati rais anaingia hawatakuwa na nafasi ya kuchangia hiyo hotuba. Lakini mimi maoni yangu ni kuwa kama ushindi wa rais bado haujakubalika kwa CHADEMA ina maana rais huyu hana credibility ya kutoa hotuba bungeni mbele ya wabunge wa chadema na hivyo hakuna haja ya kuisikiliza wala kushiriki katika mjadala wa hiyo hotuba.

Wakati wa kampeni watanzania wengi walijitokeza kuunga mkono chadema na wanasubiri nini kitafanywa na viongozi wa chadema. Wengi wako tayari kwenda kudai haki zao kwa maandamano ya amani kama viongozi wakisema wafanye hivyo. Imani yao kwa chadema bado ni kubwa. Viongozi wa chadema hawana budi kusikiliza sauti ya wafuasi wao. Kutotambua matokeo ya kura za rais ni hatua nzuri lakini lazima watu waone kuwa viongozi wanamaanisha hivyo kwa kuwataka wabunge kutoshiriki katika kusikiliza na kuchangia hotuba ya rais ambaye ushindi wake ni wa mashaka.

Kushiriki au kutoshiriki kwenye hii hotuba ya Kikwete ni mtihani wa kwanza kwa viongozi wa CHADEMA mbele ya wafuasi wake. Chama kinatakiwa kionyeshe kiko sambamba na wanafuasi wake. Wafuasi wengi waliojitolea kupiga kura na hawakupata haki yao bado wanaumia kwa kutotendewa haki. Viongozi wa CHADEMA lazima waangalie hili kama bado wanataka support ya wafuasi wao.
 
Ahsanteni wanaJF mimi maoni yangu ni kwamba tumewachagua wabunge wa chadema ili kutuwakilisha bungeni. Na ni lazima kazi hiyo waifanye maana wasipofanya 2015 watakuja hivyo vyama vidogo vya sisiem watasema wabunge wa chadema hawajafanya kitu na wapiga kura hawataelewa kama walikuwa wanasusa mikutano.

Issue hapa ni kuhakikisha kuwa Dr. Slaa asikubali matokeo wala asitokee kwenye shughuli yeyote inayomhus rais wa NEC.

Kumbuka kuna watu kibao wa CUF, CCM na wasio na vyama walitupa kura Chadema sababu ya SERA NZURI YA CHADEMA kama Makazi Bora, Elimu Bure, Afya Bure na kushughulikia mafisadi wa nchi hii.

Kwahiyo mimi naomba wabunge wote wa Chadema wawe kama Slaa wa 1995 hadi 2010 kuing'ang'ania serikali na Mafisadi kwa kwenda mbele.


Peoples Power
 
HISIA KALI

Kweli una hisia kali, umesema kweli kuwa wananchi waliowapigia kura Chadema walilala nje wengine zaidi ya siku tatu kulinda kura za rais na wabunge. Najua walisononeka sana kusikia kura zao walizozilinda zimeibiwa baada ya kufika Dar (NEC) lakini walifarijika kidogo baada ya kusikia Chadema imeyapinga matokeo.

Sasa what is the NEXT move, wanasubiri kuona ni kitu gani chama kitafanya, Chadema inatakiwa ionyeshe iko pamoja na mawazo ya wanachama waliojitolea kupiga na kulinda kura bila ya kufanya hivyo nina hakika watatuvunja sana moyo.

Sisi wanachama tulikuwa na uwezo wa kuzilinda wakati zikiwa bado vituoni lakini hatukuwa na uwezo wa kuzilinda zilipofika NEC, sasa ni jukumu la Chama kuonesha na wao kama chama wanazilinda/wanazidai kwa vitendo na si kwa kuahidi majukwaani.

Angalizo kama Chadema na wabunge wanaogopa ku risk kwa kitendo tu cha kutoka nje wakati wa hotuba ya Kikwete kwa sababu yeyote ile ni vipi wanachama wao waendelee ku risk maisha yao usiku na mchana kuwalindia kura zao vituoni? THINK.
 
Isiwe kususia hotuba ya Mh Rais tu bali pia wasusie posho zote zinazohusiana na ubunge, na kama vipi wasihudhurie vikao vya bunge; watulie huko majimbon kwao na wapiga kura wao wakifanya shughuli za maendeleo ya jimbo:sorry:
 
CUF, NCCR, UDP na TLP wameshaunda kambi yao ya upinzani wakisubiri CHADEMA wa boycot.....
 
Dawa ni kuonyesha uwezo wa kutetea hoja na kuzichambua za wabunge wa chama tawala. Wengi wao ni watu wa starehe KAMA KOMBA MZEE WA TOTZ. HAWANA MCHANGO WOWOTE BUNGENI. THEN WE WILL SEE THE CHANGES.
 
Leo ni zaidi ya wiki moja tangu Dr. Slaa atangaze kutokutambua matokeo ya urais yaliyotangazwa na tume. Wengi wetu tulitegemea ya kuwa, baada ya hapo angelielezea umma wa watanzania ni hatua gani anazotarajia kuchukua kukabiliana na hali hiyo. Lakini mpaka sasa tunaona ni kimya. Kwa wengi wetu ukimya huo umesababisha tujione kuwa ni kondoo hasiye na mchungaji. Katika hali hiyo, natoa rai kwa Dr. Slaa, kuelezea bayana msimamo wake wa sasa kuhusiana na kutangazwa kwa JK kuwa mshindi wa
kinyanganyiro cha urais. Ingelikuwa vyema kauli yake hiyo ikatolewa kabla ya ufunguzi wa bunge; kwani itakuwa kichekesho, kuendelea na msimamo wa kutotambua uchaguzi wa rais huku wabunge wa chadema wakashiriki katika hotuba ya ufunguzi itakayotolewa rais aliyotokana na uchaguzi unao upinga. Naomba kuwakilisha.
 
Mkuu hilo umenena. hata miye nimekuwa naumiza sana kichwa kutafuta majibu sipati. Je ukimya huu unatokana na nini hasa? Je kuna vitisho labda au kulikoni hata sijajua. Tunaomba kweli Dr. utupatie msimamo wako maana sie bado tuko pamoja nawewe. Tamko lako tunalisubiri na hatujakata tamaa maana kukata tamaa ni dhambi kubwa.
Ahsante nawasilisha
 
Tatizo sio kutoa tamko kinacho hitajika hapa ni mikakati yakulikomboa taifa ambalo limeporwa haki yakugawana keki ya uhuru wetu kwa pamoja.Mikakati makini haiwezi kubuniwa ndani ya wiki moja au mbili kama tunavyo hitaji kutokana na hasira za kuibiwa kura,Tunahitaji kuwa na mikakati ambayo nimadhubuti kwani kuibiwa/kuporwa kwa utawala wakizalendo umesha fanyika hakuna namna unaweza ukapinga wala huwezi kwenda mahakamani.Dr. Slaa ni rais wetu anatakiwa kutujari pia vinginevyo ana weza akatuingiza kwenye maangamizi,anatakiwa kufanya kazi ya ziada kupitia chama chake kwamanufaa yetu sote na ya kudumu sio ya mda mfupi kwania ya kutufurahisha.

Mimi nina hakika kabisa kuwa Dr. Slaa ana mikakati madhubuti ambayo haitakiwi kutangazwa mapema kumbukeni hii nivita dhidi ya ubadhilifu na haki natuna hitaji kushinda vita hii bila kumwaga damu.Mambo mazuri hayataki haraka acha kwanza vijana waape,wakae pale mjengoni wa anzishe hoja wakati Dr Slaa akizunguka nchi nzima kushukuru walio mpigia kura, hayo nimaono yangu katika kimya hiki
 
Kwa mujibu wa katiba ya TZ Dr. Slaa ndio amemalizwa, Tume ya uchaguzi ikishamtangaza mshindi hakuna chombo chochote kinachoweza sio kubatilisha matokeo bali hata kuchunguza kama kulikuwa na kasoro au la. Hili ni tatizo kubwa la katiba yetu, ndio maana mzee amekaa kimya, hajui afanye nini. Wapinzani ZNZ walikwama hivi hivi mwaka 1995, 2000 na 2005. Mwisho waliishia kupita kwa wafadhili kuwahabarisha juu ya wizi katika uchaguzi, hatimaye wafadhili wakapunguza misaada kwa Tanzania kama munakumbuka vizuri. Kwa msingi huu ndio maana jamaa wa CUF mara hii wamekuwa wapole wakijua kuwa hawa jamaa wana mpini na wapinzani wameshika makali.
 
Well noted Dr. Thanks alot.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…