Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,904
- 1,064
Dawa ya huyu kilaza ni kutomjibu lolote! Yuko jukwaa ambalo hajui anafanya nini!kama posho si issue kubwa kwa chadema, tunaomba ile ahadi ya elimu bure ianze sasa kwa michango ya wabunge wenu kusomesha angalau watoto mayatima ktk majimbo yao ndipo kauli ya posho sio issue iwe ni kweli!!!
Mnajua sometimes huwa nawaita wavivu wa kusoma michango mingi ya JF la sivyo husingeweka post yako hii hapa kwa tamko alilotoa Dr. Chomoa hapa kuona updates: https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-mbowe-marando-slaa-zitto-lissu-mnyika-2.htmlMkuu hilo umenena. hata miye nimekuwa naumiza sana kichwa kutafuta majibu sipati. Je ukimya huu unatokana na nini hasa? Je kuna vitisho labda au kulikoni hata sijajua. Tunaomba kweli Dr. utupatie msimamo wako maana sie bado tuko pamoja nawewe. Tamko lako tunalisubiri na hatujakata tamaa maana kukata tamaa ni dhambi kubwa.
Ahsante nawasilisha
Basi watoke mmoja mmoja kama enzi zile akifundisha mwalimu ambaye wanafunzi wamemkataa. waondoke mmoja mmoja mpaka wabaki sisi em A na BKama Wabunge wa CHADEMA watatoka as individuals sina tatizo na hili. lakini kama watatoka wote as CHADEMA ina maana nafasi yao kama opposition katika kikao hich haitakuwepo.
Kwa mujibu wa kanuni nadhani wanaweza kupewa BAN. Then, where will we be heading?
Jamani, haya maneno kweli yanatoka ktk kichwa chenye mvi!Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.
Hata mimi nawategemea wafanye kama walivyofanya wajumbe wa baraza la wawakilishi kupitia CUF mwaka 2005, Karume alipoingia kuhutubia, wenyewe wali match out kuonyesha ulimwengu kuwa aliiba kura na si raisi halali. Wakifanya vinginevyo na ukimya uliopo sasa sisi wananchi tuliowaamini na kuwashabikia hatutawaelewa.
ni muhimu kwa DR W P SLAA kusubiri hadi apate taarifa zote muhimu ndipo atoe statement. Kuhusu wabunge kususia kikao au hotuba y rais huko ni kupot6ka kabisa. Tena nina wasiwasi wanaotoa wazo hilo wametumwa na CCM. Plz CHADEMA msifanye hivy6 kamwe
Luteni,
Thanks a lot. Napenda kukushukuru sana. Napenda tu nikuhakikishie kuwa Chadema is not just waiting for something to happen. i) Tulitangaza kutotambua matokeo na kutomtambua Rais aliyepatikana kwa kura kuchakachuliwa. ii) Chadema hatukuhudhuria Kutangazwa kwa matokeo na wala kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais. Maana yake tulikuwa tunapeleka ujumbe mzito kwa Rais aliyepatikana kwa mchakato usio halali na kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyokiri hadharani kuwa "ilifanya makosa mathalan waliponipa kura 3,789 iliyotangazwa na Judge Lewis Makame badala ya 22,021 iliyotangazwa na RO Geita. (Hatimaye walirekebisha). Maeneo mengi yalitangazwa kwa sura hiyo, japo hayakurekebishwa. Hali hii ni dhahiri iliashiria kuwa jumla ya kura za Dr. Slaa zilizokuwakitangazwa na Tume,ilikuwa au inabadilika au haifanani na Kura zilizotangazwa na RO katika Wilaya husika. Kasoro hizi baadhi zilirekebishwa wakati wa kujumlisha matokeo ya jumla, hivyo kasoro hii isiporekebishwa sura ya kura halisi ya nchi hii haiwezi kuwa sawa.iii) Tulilalamikia kubadilika badilika kwa idadi ya Waliojiandikisha kupiga kura mathalan kabla ya uchaguzi Tume ilitangaza idadi ya Wapiga kura 19,670,631 na siku ya matokeo ilitangaza idadi ya waliojiandikisha kuwa 20,137,303. Tumehoji tofauti hii hadharani. iv) Tumehoji idadi ndogo sana ya Wapiga kura 8,626,283 kati ya au 19 Millioni + au 20Millioni +) na kusababisha kiongozi wa nchi yenye watu zaidi ya 43 Millioni kuchaguliwa na idadi ndogo tu ya wapiga kura 5,276,822 kati ya wapiga kura halisi 8,398,394 tu. Hali hii inaashiria nini katika Governance? Hivyo kwa hoja hizi Chadema haikusubiri tu ...jambo literemke from heaven.
Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.