Mbowe: Mgomo wetu umezaa Katiba

Mbowe: Mgomo wetu umezaa Katiba

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetamba kuwa hatua ya wabunge wake kugomea hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa Bunge mwaka 2010 ndiyo imezaa mchakato wa Katiba mpya.

"Licha ya ulimwengu mzima kutoelewa na kutushutumu kwa kitendo hicho, lengo letu lilikuwa ni kuishinikiza serikali ya CCM ikubali kufanyika kwa mchakato wa kuanzishwa Katiba mpya ambayo ndiyo njia pekee ya kuelekea katika ukombozi wa wananchi wanyonge," alisema.

"Baada ya kususia hotuba hiyo na kisha maandamano, Rais Kikwete alikubali kukutana na viongozi wa vyama kikiwamo CHADEMA, kwa lengo la kujadiliana na kukubaliana muundo wa uanzishwaji wa mchakato huo," alisema.

Mbowe alivionya vyama vya siasa kutouchukua mjadala wa Katiba katika sura ya kisiasa zaidi, badala yake alivitaka viwe nyenzo ya kuwezesha wananchi kuandikwa kwa Katiba mpya.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, wakati akihutubia wananchi wa mji wa Kahama, mkoani Shinyanga ukiwa ni mwendelezo wa mikutano ya chama hicho kujadili rasimu ya Katiba mpya katika mabaraza yao.

Chanzo: TDaima.
 
Back
Top Bottom