Mbowe Miaka Mitano ni Kipi Atakifanya Kilichoshindikana Kufanywa Miaka 20?

Mbowe Miaka Mitano ni Kipi Atakifanya Kilichoshindikana Kufanywa Miaka 20?

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
12,096
Reaction score
15,393
Mbowe kaahidi ataachia uongozi baada ya miaka mitano ifuatayo endapo atachaguliwa. Inafahamika ahadi ya kuachia uongozi alisha ifanya huko siku za nyuma; lakini kadri miaka ilivyo songa, matokeo ya uongozi wake yanazidi kufifia na kuonyesha dalili za kuwa anaifanyia kazi CCM zaidi kuliko kazi ya kuiondoa madarakani CCM hiyo.

Sasa, katika ahadi yake hii mpya ya kuachia madaraka baada ya miaka mitano ijayo, hajaeleza kinaga ubaga sababu hasa zinazo mfanya atake kuendelea kwenye nafasi ya uongozi wa chama.

Je, anatarajia katika miaka mitano hii atafanya miujiza gani kuifanya CHADEMA ishike madaraka; au hilo sasa siyo lengo la chama hicho?

Anataka kwenda kuanza upya mazungumzo ya kupatikana kwa Katiba Mpya; kwa kutumia njia zipi ambazo hakuzitumia kabla na baada ya kuingizwa kwenye msitu wa "Mazungumzo ya Maridhiano"?

Lakini, kinacho jitokeza zaidi ni kuwa Mbowe anayo mipango ya kushirikiana na Samia katika miaka mitano hii, bila kujali kama Samia atakuwa amechakachua kuendelea kwenye nafasi hiyo. Inazidi kuweka mashaka makubwa sana kama makubaliano ya maridhiano hayakuwa ni kuwa na ushirikiano wa aina hii; pamoja na kwamba amekwisha onyeshwa wazi kuwa ahadi alizo pewa ni hewa tupu; kama ilivyo jidhihirisha kwenye uchafuzi wa Serikali za Mitaa.

Yaliyo wazi kabisa, ni kuwa katika miaka mitano mingine ya Mbowe kukiongoza chama, uongozi huo hautakuwa na ushawishi wowote toka kwa wananchi, kwa hiyo chama hakitakuwa na ushawishi wowote wa maana kwa wananchi kuungana na chama hiki.

Itoshe tu kusema kuwa, mnufaika mkuu wa kuendelea kuwepo kwa Mbowe kama Mwenyekiti wa CHADEMA ni Samia. Mbowe anawaongezea miaka mitano waTanzania chini ya utawala wa Samia. Ni yeye pekee, na mshirika wake huyo wanaojuwa sababu ya kufanya hivi.

Mbowe kajivuruga sana. Hata hashtuki anavyo shangiliwa na hao anao wafanyia kazi?
 
Ukusikia aliposema amegundua wana umuhimu wa kuwafundisha watu siasa.

Amegundua kuna watu hawajui mipaka ya internal na external fight ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo anawajibu wa kuwapika wanachama wao.
 
Uchu wa madaraka tu. Anaona yeye ndio mwenye haki ndani ya CHADEMA .
 
Ukusikia aliposema amegundua wana umuhimu wa kuwafundisha watu siasa.

Amegundua kuna watu hawajui mipaka ya internal na external fight ndani ya vyama vya siasa.

Hivyo anawajibu wa kuwapika wanachama wao.
Yaani imemchukua zaidi ya miaka 20 kugundua hilo tu, la "kuwafundisha watu kujuwa mipaka ya 'internal na external fight'"? Huyu huoni kuwa atakuwa ni mwalimu mbovu sana?

Mbowe aseme tu ukweli wake. Anakitumia chama kufanyia biashara kama alivyo bainisha mwenyewe kuwa hiyo ndiyo shughuli yake muhimu. Hii ni biashara haramu.
Huwezi kuchezea hatma ya nchi na wananchi wake kwa manufaa binafsi.
 
Back
Top Bottom