Mheshimiwa Mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe na Makamu mwenyekiti Tundu Antipas Lissu nianze kwa kusema ninawaheshimu sana.
Mmepigwa mawe mengi sana ya maneno ya kisiasa, mmevumilia mengi sana, mmenyang'anywa hata mali zenu, mmeshikiwa mtutu wa bunduki. mmewekwa mahabusu kwa manufaa ya akina Msigwa ambao wamelambishwa asali na Sasa wamewageuka.
Pandisheni mikono yenu juu mwambieni Mungu ahsante kwa kuwapa uhai na kisha yeye atashughulika na wasiokuwa na shukrani. MSITENGANE nanyi mtaingia kwenye mkumbo wa laana. Maana kuna wengine wameumizwa hata wengine kupotea uhai wao Kwa kuwaamini ninyi.
Katika watu ambao sikutarajia kabisa kuwa watakuwa hivyo Msigwa na Peneza. Ukisikiliza maneno yao, vijimambomambo vyao, unafika mahala ambapo sipo.
Mbowe we ni kaka yangu kwa umri wangu na wako naomba unisikilize. Jenga chama wamehama waliokuwa na nguvu kubwa kuliko hao wanaobwabwaja Chadema ipo palepale. Umekijenga chama ni taasisi kubwa hata wao wanajua.
Nilitegemea wanaowasema vibaya wasingekula matapishi yao. Waliisema sana CCM na ninaamini wameamua kutumika na wamekubali kutumika kama paper of toilet, wenye Chama wanawachora tu. Maana tabia za CCM hawawezi kwenda kuzibadilisha ila wameamua kuzisapoti Kwa vipande vya fedha.
Najua mnaumia watoto mliowalea Kwa jasho na damu out wanahangaika kuwatoa roho ya ki-siasa lakini ninachooamini kama wako sahihi Mungu atawasimamia waendako. Lakini kama andiko la kwenye waraka wa kwanza wa Timotheo 6:10 linatimia kwao hakika hawatafika mbali. Binadamu inatakiwa uwe na moyo wa shukrani angalau hata kama mzazi wako pengine kakosea kidogo ni binadamu . Si kama wanavyowafanyia. Bila Chadema wasingebinua midomo hivyo.
CCM kuna watu wengi waliohangaika na chama tangu miaka ya 77 hawajawa maarufu kisiasa kiasi hicho. Wao miaka ya 95 tu umewapa umaarufu wamekugeuka "shukrani ya Punda mateke".
Hivi wanasiasa kuna sababu ya kuwa na dini au dhehebu? Nachelea kuamini hivyo. Mbona Wana dini zao halafu wanawatenda hivyo?
Kwa wananchi wa kawaida tumepata faida kubwa sana kuwapo vyama vingi na hasa chama chenye nguvu kama Chadema. Wametumwa mamluki wengi sana Chadema ife Kwa ulaghai wao bila nguvu zenu chama kingekuwa chali kama vingine. Kupitia vyama vingi tumepata manufaa nataja machache yafuatayo:-
1. Uthubutu wa kufikisha malalamiko yetu Kwa watawala tukiwa na shida maana hatukuzijua haki zetu. Hatukujua utawala wa kisheria.
2. Watawala walikuwa wanatekeleza miradi wakijisikia walikuwa wanapenda kutumia neno tuko kwenye MICHAKATO. Mpaka miaka 10 unapita wanachakata.
3. Tulikuwa tunawekewa kivuli na mtu tuchague NDIYO au HAPANA.
Mimi ninaunga mkono sana vyama vingi. Wanaotaka Mbowe na mwenzio Lisu mkose nguvu wanataka kuturudisha kwenye mambo hayo niliyotaja na mengine mengi.
Ninachoowamba umoja wenu na viongozi wengine wenye nia njema udumu kusiwe na mafarakano mtaliokoa taifa hili na mtabarikiwa.