Mbowe namfananisha na Matajiri wa Kiafrika

Mbowe namfananisha na Matajiri wa Kiafrika

Bird Watcher

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2013
Posts
3,151
Reaction score
6,261
Wakuu, Matajiri wa Kiafrica Ni wapambanaji sana Ili kuleta ustawi wa Familia na Koo zao, Huwa hawalali Na Kiukweli hujitahidi kadiri ya Uwezo wao familia Kusimama!

Pamoja na Mazonge yote watu hawa wamejawa na Siri nzito sana na Pia ni watu ambao huishi kwa Machale muda wote

Matajiri wa kiafrika huwa hawana Mpango wa kufanya Weath transformation ndio mana unaweza kuta Mtu ni tajiri kweli kweli ila akifariki leo haipiti Mwaka tayari Familia zao zinatumbukia Kwenye Ufakara wa kutisha kabisa, Sisi waswahili husema Mali zimemfata Mhusika

Matajiri hawa hawana mpango wa kuandaa Familia zao ili Kurithi Utajiri wao huwa ni one man show kila Kitu ni yeye

Ndio naiona Picha Hii kwa FAM, Leo Mbowe anaona Chadema haiwezi kusogea mbele bila yeye kwasababu tu yeye amekuwa akitoa Vimia mbili mbili Nje ya utaratibu kufinance Harakati za Chama, Anaamini ana endurance kubwa ya Kuhimili Mikimiki Kuliko mwanachama Yoyote,

Vijana wengi tumepita kwa FAM lakini hatuoni akitoa Picha Kubwa ya wapi anapeleka chama na Succession plan yake ni kama hakuna vile, Je ikitokea Muumba akampenda? (Hatuombi iwe ivo) Je chama nacho kitakufa?
 
Back
Top Bottom