Mbowe ni mtu wa ajabu sana, migogoro aliianzisha mwenyewe kisha leo anaomba kuchaguliwa ili aunde tume kupatanisha aliowatenga

Mbowe ni mtu wa ajabu sana, migogoro aliianzisha mwenyewe kisha leo anaomba kuchaguliwa ili aunde tume kupatanisha aliowatenga

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Ukweli ni kuwa Mbowe aliamua kwa makusudi kutenga great thinkers wote ndani ya Chadema. Na kuna picha nilipost humu akiwa na machawa wake hii hapa.
20250109_170116.jpg


Ukweli ni kuwa hii picha alikuwa kwenye kikao na machawa wake hawa kuandaa mpango wa kudili na watu. Ni kwenye kikao hiki ndipo alisema Lissu na Heche hawamfai. Likaanza zengwe.

Baadae Lema alipopata hizi habari akamvaa Mbowe kuwa analopanga halifai. Kitendo cha Lema kusema hivyo nae akawekwa kwenye list. Mbowe alihakikisha watu wote wanaompinga hawapenyi kwenye uongozi kuanzia mikoani mpaka kwenye kanda maana alikuwa hataki kuvuka nao kama viongozi.

Mbowe alilewa madaraka, baada ya kuona kila anayeondoka linatungwa zengwe na yeye anapenya (Rejea walioondoka huko nyuma) akaona na hili litapita maana anahisi chama alishakikumbatia.

Sisi tulishtukia usanii wake na tukamkataa. Ameona mambo magumu anakuja na kailani kamchongo ka kuunda tume ya upatanishi! Unafanya hivyo baada ya usanii wako kugundulika? Unafanya hivyo baada ya wanachama kukataa hila zako? Kwanini hukuona haya kabla? Unahangaika kutwa kucha ulidhani ni mzaha? Chama ni mali yako? Usijidanganye hata kidogo kuwa Chadema kinaweza kuwa kikundi chako na machawa wako kuunda miradi uchwara ili mtafune fedha za chama.

Tumekugundua tukakushtukia na kukushukia ghafla kama mwewe sasa unahangaika.

Sisi kauli yetu ni ile ile kuwa hapa ulipotufikisha tunashukuru. Kwenda huko mbele hatukutaki tena ukae mbele utuongoze maana una dosari nyingi kwa sasa.
 
Mbowe akishinda atakuwa mwenyekiti wa familia yake na members wachache wa saccoss, lkn wanachadema halisi wanamtaka losu
 
Aisee! Mbowe hafai.
Huyu Mzee kwa nguvu anayotumia kung'ang'ania madaraka inashitua sana!

Miaka 21 bado unang'ang'ania?

Inanifanya madaraka niyaangalie kwa sura pana sana!
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Amekumbuka shuka wanakati kumekucha. Too late to apologise and to mend errors.
Chadema ni ya ajabu sana! Wanasema people's power halafu wana undermining majority opinions.

Huyu Mzee atasababisha watu kutoana damu tarehe 21.
 
Huyu Mzee kwa nguvu anayotumia kung'ang'ania madaraka inashitua sana!

Miaka 21 bado unang'ang'ania?

Inanifanya madaraka niyaangalie kwa sura pana sana!
Huyu mzee anatuamsha tuvione vyama vya upinzani kuwa ni miradi ya watu.
 
Mbowe tapeli sana. Ashukuru tulichelewa sana kumjua.
 
Back
Top Bottom