Samson Ngomboli
JF-Expert Member
- Oct 30, 2019
- 1,598
- 2,714
Kusema sio vibaya,ubaya unapokuja kwenye uwasilishaji yaani ukitanguliza tu mihemko na chuki maana ya kilichokusudiwa kinabadilika kuwa fujo.Kwani kuna ubaya gani kuisema serikali kama inafanya mambo ya ovyo? Unataka tuisifie wakati watu wanatekwa na kupotea, Mbunge Lissu anapigwa risasi mchana kweupe, viongozi wa vyama vya upinzani wananyanyaswa, vyombo vya habari vinaminywa, mishahara ya watumishi was umma imebanwa, n.k
Wanasiasa wengi Kwasasa,upinzani au tawala,wengi hawajui kujenga hoja na inaishia kuongea uozo tu,ulijaa unamsikiliza mtu anayejiita mwanasiasa,sijui mwanaharakati mambo anayoingea mpaka unahisi kinyaaa
Kosa lake moja tu,Mbowe anajielewa sana
Kukomaa kisiasa haimaanishi awe mwenyekiti wa milele!Kampeni yenu ya kutaka asichaguliwe tena kuwa Mwenyekiti wa Chadema imefikia wapi?? Acha unafiki
Je, ulimsikia siku alipotangaza vita ya Kagera pale Diamond?!..ni kwasababu wengi hawana utamaduni wa kujisomea, na hivyo kushindwa kuitawala lugha, na kujenga hoja.
..hata Jpm kwasababu hana hoja za kuzungumza ndiyo maana mikutano yake inakuwa na utitiri wa wazungumzaji, wakiwemo viongozi wa dini, na washereheshaji mbalimbali.
..wakati wa Mwalimu Nyerere baada ya utambulisho mfupi alikuwa akihutubia yeye mwenyewe. Na sikuwahi kumsikia akizungumzia ngono, akitukana au kutishia mtu, au akidhalilisha wanawake.
Katika hili swala la ukomavu wa kisiasa kiukweli Mbowe namsifu, hutamsikia akiisema vibaya serikali kwa utaratibu wa hovyo hovyo.
Kuna wakati huwa najiuliza kama yule Boss wa ACT wazalendo angekuwa ndio KUB sijui hali ingekuwaje?
Maana huwa anaongea lolote, popote tena bila utaratibu.
Niwatakie maandalizi mema ya Dominika.
Maendeleo hayana vyama!
Naona wewe ndio unang'ang'aniza!Naona mnang’ang’aniza conformity watu waweke vichwa chini kuhusu uongozi mbovu wa Jiwe!
Stop this nonsense mzee!
Je, ulimsikia siku alipotangaza vita ya Kagera pale Diamond?!
Idd Amin hakutukanwa siku ile?!!..nilimsikia.
..na hotuba hiyo nimeileta nzima hapa JF kwa faida ya mbumbumbu wa uvccm na kizazi kijacho.
..pia nilimsikia Samora Machel akihutubia kwa zaidi ya masaa matatu uwanja wa taifa dsm.
..huyu tuliyenaye Kiswahili hajui, Kiingereza ni balaa tupu. Hotuba zake ni matusi, kejeli, mipasho, na vitisho.
Naona wewe ndio unang'ang'aniza!
Kwani Mbowe ni rafiki wa CCM?!Naona unajenga boundaries za watu ku conduct their politics kwa kuwafanyia comparisons na kuchukua yule ambae ni friendly kwenu kama standard!
Wengine waliopo nje ya hiyo standard mnayoona ni friendly kwenu ni wabaya!
Good riddance!
Sasa mbona wewe unajiumiza na kuteseka!!Kuna watu wanalipwa kuandika chochote humu JF, wapo wengine wanashinda humu bure, na hawana kazi za kufanya, lakini hawakosekani humu.
Kafanyeni kazi msikae bure na kupoteza muda wenu, mnaobishana nao wao hiyo ndiyo ajira yao, wanalipwa.
Tumieni akili zenu kuendesha maisha, mkija humu iwe burudani tu, msijiumize sana.
Hilo la kujisomea na kujifunza wenzao walifanyaje au wanafanyaje umemaliza kila kitu..ni kwasababu wengi hawana utamaduni wa kujisomea, na hivyo kushindwa kuitawala lugha, na kujenga hoja.
..hata Jpm kwasababu hana hoja za kuzungumza ndiyo maana mikutano yake inakuwa na utitiri wa wazungumzaji, wakiwemo viongozi wa dini, na washereheshaji mbalimbali.
..wakati wa Mwalimu Nyerere baada ya utambulisho mfupi alikuwa akihutubia yeye mwenyewe. Na sikuwahi kumsikia akizungumzia ngono, akitukana au kutishia mtu, au akidhalilisha wanawake.
Hujui?Kwani lipumba na lyatonga ni ccm?
Wewe ni kiojaUmesema kweli mkuu,sijui wanakwama wapi maana ngao ya wapinzani kwa sasa ni fujo na kulia lia wapewe kura za huruma na sisi wapiga kura tunataka hoja na sio vihoja.
Sawa mkuu maoni yako yanapaswa kuheshimiwa.Wewe ni kioja
Lyatonga ni tlp na lipumba ni CUF au hujui hilo mkuu?Hujui?
😄👍Kosa lake moja tu,
Kubadili gia angani, ndoto zetu zikaishia hewani.
Otherwise Mbowe is wise, full of wisdom.
If it had depended on my advice, he would have seen heaven's kingdom.
And it's so nice, his name is related with freedom.
Ahaah! nilikuwa natest kama naweza kughani kwa kimombo.