Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Baada ya onyo la Polisi dhidi ya Wanachama wa CHADEMA waliodaiwa kuwa na mipango ya kuvamia vituo vya Polisi, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema hatua hiyo ni shambulio jingine la kizushi na chuki dhidi ya CHADEMA na viongozi wake na kuwa ni mkakati wa makusudi wa Polisi wa kutafuta kisingizio cha kukamata na kutesa Wanachadema kwa taarifa toka vyanzo vya uongo.
Aidha, amewataka Polisi kueleza hicho kikao cha Zoom kilifanywa na akina nani na kilikuwa na wajumbe gani!
Soma: Kuelekea 2025 - Jeshi la Polisi: Tumepata taarifa CHADEMA wanapanga Maandamano na Kuvamia Vituo vya Polisi Dar kwa wakati mmoja
Hata hivyo, amesema kuwa pamoja na CHADEMA kutokufanya kikao kinachodaiwa, Polisi itambue na kuheshimu haki ya makundi mengine ya kijamii kujadili utekaji nchini.
Amefafanua kuwa “Tuhuma hizi ni mkakati wa kukwepa kuueleza Umma walipo Viongozi wa CHADEMA, Deonis Kipanya, Deusdedith Soka, Jacob Mlay na Mbise”
Amemsihi Rais Samia kuelekeza Vyombo [vya Dola] vyake vieleze walipo vijana hawa na wengine wengi wanaoendelea kupotea nchi nzima.
Utekaji ni uhalifu na kamwe hauwezi kuwa mkakati wa kulinda amani ya nchi.