Mbowe; Recruiter Bora kuliko hata TAI!!??

Mbowe; Recruiter Bora kuliko hata TAI!!??

residentura

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,146
Reaction score
11,434
Huyu ndugu yangu Freeman Mbowe naamini ndiye recruiter bora kwa miongo 3 katika nchi hii (kwenye upande wa siasa).

Kwa nini serikali/system isimchukue na kumpa kitengo cha kutafuta vijana wenye uwezo, kuwapika na kisha tukapata wakina Lissu wengi, wakina Heche wengi, wakina Mnyika wengi, wakina Wenje wengi, kwa ajili ya kulitumikia taifa kizalendo!!?

CCM, ambayo imekuwa ikiunda serikali tangu tupate uhuru, haina mpango mkakati mwema wa kuibua vijana wenye vipawa na kuwatengeneza kwa ajili ya kulitumikia taifa kizalendo.

Tumeona vijana wengi walioibuliwa na kupikwa na CHADEMA (hasa hasa Mbowe binafsi), wamekuwa na uwezo mkubwa wa ujengaji hoja na kiuongozi.

Kwa nini tusimtumie Mbowe kitaifa katika kuibua vijana wengi na kuwapika kwa ajili ya kulitumikia taifa!!??

Mbowe amejitahidi sana kwenye hili la kuibua vijana wenye vipawa vya uongozi, lakini naona anakwama kwenye succession plan kama ambavyo Waafrika wengi tunavyokwama kwenye hili.

Kwa heshima kubwa naelekea kuonana na huyu ndugu yangu ili kumshawishi atengeneza mkakati wa kuendeleza ule mpango wake wa kuibua vijana wenye vipawa mabalimbali na aachane na hizi active party politics, hasa uongozi.
 
Mjasiliamali wa siasa za Tanzania

Mbowe ana tofauti gani na Mrema na Lipumba ?

bora hata cheyo ila sio Mbowe aisee

Mbowe toka alivyoruhusu Lowassa kwenda chadema isee niliona ni ni kweli form six zero!!
 
Kwenye uchaguzi wowote minyukano inaruhusiwa
Bora kunyamaza maana kula yako ipo Chadema. Wewe nikati ya watu 20 aliowasema Lissu kuwa mnalipwa mishahara na Chadema. Hivyo ukimya wakati huu ni muhimu la sivyo akiingia Lissu, unarudi kijiweni. Huku kijiweni si pa kukimbilia maana tunamenyeka ajabu
 
Wewe hunijui yaani! Wanaonijua humu JF wanaendelea kukudharau kila siku.

Ukitaka kuwa mwandishi mzuri hapa jf usishambulie individuals, sitaki kuamini kwamba ulijiunga jf ili kunishambulia mimi kwa hoja za uongo tu baasi, yaani huna lingine lolote la kuandika?

Mimi siyo masikini wa kulipwa si na Chadema bali hata serikali yako, nimeanzia siasa hizi nikiwa nje ya Nchi, sikuanzia Chimwaga au Chamwino.

Usishindane na aliyejaaliwa utadhalilika
 
Wote tupo makapuku tu, unachonizidi ni kuwa chawa wa Mbowe tu
 
Back
Top Bottom