Mbowe sawa lakini siyo man of the hour.

Mbowe sawa lakini siyo man of the hour.

El Roi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
297
Reaction score
537
Moja ya mambo ambayo huwa ni ngumu kwa mwanadamu, " ni kujua muda na nyakati sahihi kwenye kutofanya au kufanya aina Fulani ya mambo.

Nyakati au muda Fulani uamua kifanyike kipi na kipi kisitendeke.
Bahati mbaya binadamu wengi huwa hawajui wakati upi ( season) unafaa au haufai.

Kwa kawaida mwanadamu akikolewa na jambo basi udhani kawaida ndo Sheria. Kuna wakati kawaida SI Sheria.

Na kwa kujua Hilo ndo maana kukawa na usemi usemao, Kila mcheza muziki mzuri hujua wakati Gani aliache jukwaa. ( A good dancer knows when to leave the stage).
Maana ya usemi huo ni kuhusia kwamba ni vema mchezaji wa muziki akishuka jukwaani wakati bado watu wanampenda.

Kwa kile kinachoendelea Chadema juu ya nani awe mwenyekiti wa Chadema, naona mbowe ufahamu huu umemkosa wa kushuka jukwaani mapema.

Sijui kwa Nini jambo rahisi kiasi hiki limemshinda. Hapa Sasa ndo naona utamu wa madaraka unavyolevya. ( Absolute power corrupts absolutely). Mbowe ameshindwa kujua huu siyo wakati wake na matokeo atayaona.

Mbowe kaongoza chama hiki muda mrefu, kwa vigezo vyovyote muda umemtosha na amechoka.

Mbowe kaweka input ya Kila namna kusaidia chama hiki, ukweli usemwe in put yake sasa inatosha.

Exposure na knowledge ya namna ya kufanya siasa za wakati huu, haziko kabisa tena na Mbowe. maana kwa mazingira yoyote, he is completely tired .

Jambo ambalo watu huwa hawajui, ni kwamba , viongozi wote unaowaona kutoka Kila sekta, huwa kwa kawaida ni wachovu. Majukumu, kupanga namna ya kuendesha mambo na mambo ya Kila siku ya taasisi huchosha sana.
Sembuse mtu aliyeongoza miaka 20, hakika amechoka.

Huu ulikuwa wakati wake wa kuliacha jukwaa kwa heshima. Mambo aliyoshindwa kuyafanya miaka 20 ya Uongozi wake hawezi kuyafanya kwa miaka hii 5 anayogombea Tena.

Vinginevyo anataka kwenda tu kuongeza umri Ili asitaafu akiwa na umri kama wa Mtei na Makani miaka 68 na 69 kama alivyosema Leo. Maongezi yake tu hayo yanaonyesha uchovu alionao .

Naiona aibu ambayo Mbowe anaitengeneza Sasa hivi, awe ameshinda uchaguzi au ameshindwa.

Akishinda ataitwa kinganganizi na mtu aliyejimilikisha chama, lakini baya zaidi atashindwa kuongoza substantively maana he is already out of touch and mediocre as it comes to matters leadership.

TL ndo man of the hour. Huyu ndo kiongozi wa wakati. ( Man of the hour). Njoo huku mtaani uone vibe lake na anavyoungwq mkono na watu!!

A serious lawyer , scholastic on modern stuffs, exposed to many angles of knowledge, good self explanatory, Intra relational ability and the most feared politician.

Wakati mwingine tuwe tunajiuliza walau kijinga, kwa Nini aliokoka na shambulio lile baya. Naomba niwaambie for such this hour.

Nilimalizie kwa kusema, mbowe sawa, lakini SI mtu wa wakati. Na Kila muda huwa una mtu wake.

Sitaki kuwa a doom prophet, ikitokea mbowe akashinda atapata shida ambazo hajawahi kuziona za kiuongozi na hakika atachoka vibaya na atachukiwa kuliko. Angefahamu kwamba wakati wake umekwisha " angetunza heshima yake".

Mbowe ni mtu mwema, amesaidia chama, amejitolea wakati wote na hata kwangu Mimi Nampa credit. He is such a gentleman lakini likija suala la Uongozi muda huu, He is not a man of the hour.
 
Back
Top Bottom