Kuna watu hapa hawasalimiani, Lema mpaka anakimbia anaogopa kugombea kanda, shughuli ya mitandaoni hiyo, katandikwa mtandaoni mwenyekiti wa kanda mwenye mamlaka ya kanda yake, kiongozi wenu, wako viongozi ambao ni wa kawaida kabisa wa majimbo, wa wilaya, wananchama wa kawaida wanaweza wakamtukana wakamdhililisha na familia yake hii haiwezi kukubalika.
Awe na makosa asiwe na makosa unapokuwa na kiongozi ambaye hamumuheshimu hawezi kuwaongoza kwenye safari yenu, Naye vilevile kama Lema mwenyeiti wa kanda anapaswa kujua kwamba ana vijana wake huku chini wakikosa adabu wakikosa adabu, lazima awaunge awakusanye ni wake, mimi nawakusanya wote pamoja na matusi yote nayopigwa, Tunahitaji amani irejee Arusha, sitaki nije Arusha niambiwe mimi ni wa kundi fulani mimi sina kundi kwa sababu wote ni watu wa CHADEMA na wote ni wangu.
Nitaongea na Lema kwanza ni mdogo wangu mimi ni kaka yake kama alivyosema ni kweli wote ni wa njia moja, nikigombana na Lema kwenye chama Mama yake Mzazi ananipigia simu, nikigeuka Baba yake ananipigia simu umeamkaje mwanangu, haniambii habari za Lema ananiambia mwanangu umeamkaje, sasa wewe unafikiri hiyo maana yake nini? Mko salama huko? Umeakaje leo? Ameshasikia kwenye mitandao huko watu wanapiga Mbowe na Lema hawaelewani.
Siwezi kugombana na Lema siwezi kugombana na Amani, siwezi kugombana na kiongozi yoyote wa chama hiki, wote ninyi ni familia yangu tuna malengo ya pamoja. Nilikuwa nakuja Arusha yaani nikija Arusha, yaani nikija Arusha tunatoka kwenye mkutano tunakwenda mahali tunachoma nyama tunakula tunaongea tunapendana, Kulikuwa na upendo Arusha, kila mmoja alikuwa anakuja anatoka Tanzania anakuja Arusha anatamani ile love ya Arusha, mmeiharibu ile love ya Arusha lazima tuorejeshe.
Pia soma:
- Kuelekea 2025 - Mbowe: Kuna Watu wanasema Nina mgogoro na Tundu Lissu nawaambia Watasubiri sana, Chopa inaanza operation Karatu na Nitakuwa na Tundu Lissu!
- Kuelekea 2025 - Ni kweli Mbowe hawataki Lissu, Heche, Lema, Msigwa na Wenje ndani ya CHADEMA?
- Ukomavu wa Freeman Mbowe unashangaza! Pamoja na kushambuliwa na wengi lakini hajawahi kulipa kisasi