Pamoja kuwa na mtizamo tofauti na ulichoandika, lakini kwa asilimia mia nakubaliana na naiamini hiyo kanuni uliyoinukuu.
HAIWEZEKANI Leo CCM wakawa ndiyo mashabiki wa Mbowe kwenye uchaguzi huu.
Inawezekana wanatumia kanuni nyingine ile ya "wagawanye ili uwatawale" au wanaanda sherehe anguko la Mbowe likitokea.
Lakini pia nina hakika Lissu akichaguliwa, CCM watutumia mifumo ya kidola kuwaonesha CHADEMA walikosea kumchagua Lissu kuwa Mwenyekiti wao.
Muda utaongea si kitambo kirefu kutoka Sasa.