Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 735
- 1,467
Na. Robert Heriel.
Leo baada ya kutoka ofisini nikaamua kujumuika na Ulimwengu kupitia Mitandao ya Kijamii. Hapo nikaona taarifa moja ambayo ilinifanya nitafakari sana.
Niliona Video moja yenye maandamano ya vijana wa CHADEMA yaliyoongozwa na Ndugu Daniel Naftali ambapo kundi hilo la Waandamanaji limeamua kumchukulia Fomu ya kuwania Uenyekiti wa CHADEMA taifa.
Kama Mbowe atapata nafasi ya kuwania nafasi hiyo basi itakuwa ni mara ya tano kwake kushika nafasi hiyo nyeti katika chama hicho.
Moja ya Dosari ambazo chama cha CHADEMA kinajaribu kuwaonyesha Watanzania ni suala uhaba wa Viongozi wake wa juu.
Sitaki kuamini kama CHADEMA haina mtu mwingine wa kukiongoza Chama hicho zaidi ya Mhe. Freeman Mbowe.
Dosari hii ilijitokeza hata Mwaka 2015 ambapo CHADEMA kilimpokea Lowasa na kumpa tiketi ya kupeperusha bendara kwa kuwania uraisi.
Lile kwangu japokuwa sina uzoefu na siasa lakini nisingeshindwa kuelewa kuwa lilikuwa ni kosa kubwa ambalo litaigharimu CHADEMA miaka kumi kama sio ishirini ijayo.
Mbowe amebakiza jambo gani ambalo atalifanya kwa mara ya tano. Kwa muono wangu. Mbowe hana alichobakiza. Labda kama anataka kuharibu Rekodi yake nzuri ya kukijenga Chama hiko ambacho kwa sasa ni Chama Kikuu cha Upinzani.
Mbowe unapaswa upumzike uwe kama Mshauri wa Chama. Nafasi hiyo itakuwa muhimu yenye manufaa kwa Chama.
Ikiwa umeongoza zaidi ya miaka kumi na tano lakini unaona hujafikia lengo basi hutoweza kufikia malengo kamwe bali unachokitafuta ni kuharibu hata mazuri uliyoyafanya.
Labda Mhe. Mbowe nikuambie tuu kuwa kwa Utawala wa Magufuli huna ubavu wa kukabiliana naye. Hilo limedhihirika wazi wazi Kimbinu, kimkakati, Kipropaganda na kinguvu.
Magufuli kama hasimu kutoka Chama tawala amekumudu kikamilifu. Sijajua umekusudia au ndivyo ilivyo kuwa umezidiwa.
Mhe. Mbowe kwa staili unayoendesha chama cha CHADEMA ni Bora upumzike tuu kwa maana chama kitakufia mikononi. Ukileta mchezo hiyo Mwakani usishangae ukakosa wabunge hata kumi kutoka chama chako.
Mbowe kwa Sasa huna mbinu muhimu kukabiliana na Magufuli ambaye amekupiga katika maeneo muhimu. Hakuna sehemu aliyokuachia pumzi.
Sijajua ninyi mnaotaka Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti mnamaono gani. Lakini nawahakikishia. Mbowe hana mbinu za kuikabili CCM.
CHADEMA ikitaka iwe chama kinachoeleweka inapaswa ichague kiongozi ambaye hatakuwa analalamika na kutoa maneno matupu.
CHADEMA mnapaswa mchague viongozi wanaoweza kuchukua hatua na kupambania kile wanachokiamini ni manufaa katika taifa.
CHADEMA inahitaji mtu kama Robert Chagulani almaarufu kama Bobi Wine.
Kama Mbowe hautapumzika basi kwa mara ya kwanza nitapaza sauti kuungana na wanaosema Magufuli aendelee mpaka 2035.
Yaani CHADEMA ikijikanyaga ikamchagua Mbowe. Ninakuhakikishia Magufuli ataongoza kwa Vipindi zaidi ya Viwili. Nami nitapigia Chapuo kampeni hiyo popote pale nilipo
Kijiweni nitapiga Kampeni. Sokoni, Kanisani, Misikitini, Mitandaoni na kila pahala. Nitapiga Kampeni Magufuli atuvushe mpaka 2035.
Ninayo team ya kutosha tuu ya kufanya jambo hilo. Tayari team ya kwanza ilianza kupiga Kampeni hiyo. Mimi nilikuwa mmoja wa wanayoipinga na kuiona ni kampeni ya kipunguani.
Lakini kama Mbowe hutapumzika ati nawe kwa upofu wako ukajiona unalaziada nakuhakikishia utakuwa umefanya kosa la msingi ambalo litaigharimu Chadema.
Mimi nilikuwa na uhakika kuwa Magufuli atatawala Awamu moja tuu. Na mpaka sasa huo ndio muono wangu. Lakini kama utachaguliwa Mhe. Mbowe nakuhakikishia Magufuli atatawala zaidi ya miaka miwili.
Kama hautapumzika basi Magufuli namruhusu akimbie mpaka 2035.
Magufuli ndiye kiongozi ambaye mpaka sasa amejitahidi kufanya angalau yale niliyowahi kufikiria kuyafanya.
Japo suala la kuua Upinzani kwa nguvu anazingua sana. Na hilo nitamkemea kila mara. Lakini huko kwingine nitampongeza na kumsifu.
Magufuli tuvushe mpaka 2035 kama Mbowe hatapumzika
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300