Kwa kweli Watanzania tuna safari ndefu tena sana
Haya kama watanzania wote tulivyo wasomi na wasio wasomi, badala ya kujadili mada tunajadili watu, badala ya kujadili sera tunajadili mahusiano ya watu.
Tangia BCS Times nilikuwa naona hiki kijuwe kama sehemu ya kujadili matatizo na namna ya kuyatafutia ufumbuzi lakini naona tumepoteza mwelekeo.
Chadema iwe NGO, au chama cha siasa, CCM iwe chama cha taifa, jambo muhimu ni je tunaweza kupiga hatua kwa kupitia sehemu hizo kuondokana na maadui watatu wa maendeleo.
Nadhani hamna mtu aliyelazimisha au anayelazimishwa kujiunga na aidha CHADEMA au CCM au chama cho chote kingine bali ni mapenzi ya mtu baada ya kusikiliza na kukubali anachosikia na kuona. Yes, Chadema inaweza kuwa chama chenye chimbuko au kuongozwa na watu kutoka Kaskazini au familia moja, wanaojiunga nacho wanafanya hivyo kwa mapenzi yao. Swala la kujiuliza je undugu au ukaskazini unaolalamikiwa umezuia shughuli za chama au za wabunge na madiwani wa chama kufanya kazi zao, jibu ni hapana.
nadhani tunachofanya hapa pamoja na elimu yetu ni kuwakosea haki waTanganyika na wanachama wa vyama husika kusema eti chama cha siasi ni mradi wa kibiashara wa familia. Nadhani Tanzania tulivyo na ubinafsi kama chama hiki na vyama vingine vingekuwa miradi ya biashara ya familia fulani, sidhani kama wangewachagua wabunge na madiwani kutoka kwenye hivyo vyama.
Ndugu Tafiti, nashukuru sana kwa utafiti wako, fanya hivyo pia kwa wabunge wa kuteuliwa na kuchaguliwa wa vyama vingine hususani CCM kwa sababu ndicho kina wabunge wengi bungeni wa kuchaguliwa na kuteuliwa, halafu angalia pia nafasi za kuteuliwa. Baada ya hivyo leta ulinganisho hapa na wanaforum watajadili na kufikia uamuzi.
Kitu kingine ambacho kimeniacha hou kwenye mada hii ni kitendo cha wanaforum kuamua/kupima maendeleo ya mtu bila kutuambia vipengele walivyotumia. Ni aibu kubwa kwa mtu mwenye akili makini kutoa misemo kama "..alikuwa na maendeleo au anazingatia maendeleo lakini sasa hivi hana maendeleo.." Kila mtu ana maana yake ya maendeleo, na kila mtu anajua yaliyomuhimu kwake kufikia maendeleo anayotoka. Kama hatumpendi mtu au kikundi cha mtu tusitumie kigezo hicho kuwaamulia wengine maendeleo yao.
Kuna valid question ambazo tungependa kujua majibu yake lakini nandhani mfumo tunaotumia wa muulizaji kuuliza na kupendekeza majibu hapo hapo, ni vigumu sana hata kwa Mwendawazimu kujibu maswali kama hayo.
Jambo lingine ni tabia ya watu kuibuka na hoja mpya kabla ya kujibu utata unajitokeza kwenye hoja alizotoa awali. Haitoshi kusema mtu ni mwizi halafu polisi anakuambia nadhani siyo mwizi, wewe badala ya kumweleza polisi huyu ni mwizi kwa sababu hizi na zile, unaibuka na kusema ni mbakaji, ukiambiwa siyo mbakaji badala ya kutetea hoja na vielelezo vyako uanibuka na kusema ni msemaukweli. Kumbe kule BCS Times tulikuwa na vichwa vilivyokwenda shule kweli na tulikuwa serious.
Mzee ES, Sam,Mkandara, et al turudishe ile HESHIMA ambayo iliwafanya mpaka wa USALAMA wakeshe hapa kwani kulikuwa na hoja zenye maana na nzito, hoja ziliwafanya mpaka baadhi ya watu wa usalama wasaliti wakubwa wao na kuingia hapa kumwaga mambo.