1. Lakini wote mliohusisha matokeo yangu ya kidato cha nne na suala hili la udini kwamba nilipendelewa mmetumia wrong indicator. Na nasema hizi kwa sababu tatu: Mosi, ninahistoria ya kufanya vizuri sana katika masomo yangu kabla hata ya kwenda seminarini.
Kwa hiyo labda mnijibu, niliposhika nafasi ya kwanza mkoa wa DSM na kuchaguliwa kwenda shule ya vipaji maalumu ilboru, nilipendelewa na kanisa?Mkumbuke shule ya msingi mbuyuni niliposoma haikuwa shule ya kanisa! Pili, kati ya wanafunzi wote wa Maua seminari niliomaliza nao kwa nini ni mimi tu waliamua ‘kunipendelea' kunipa division 1.7. Why me?.
Tatu, nilipofika Tambaza na kuendelea kushika nafasi ya kwanza darasani napo palikuwa na mkono wa kanisa?. Nadhani ni vyema aliyetoa na mliounga mkono hoja hii mkakiri kwamba mlitumia mfano ambao sio sahihi!.
2. Narudia tena; sijapata division 3 pointi 17 kidato cha tano. Nilipata division 2 pointi 12. Niliposema awali Chinga amekuja tena na kusema nimedanganya. Sijui una nia gani ndugu yangu.
Utamaduni wa Forum hii ni kuwa mtu akiteleza na kutoa fact kimakosa anaomba radhi. Sasa wewe unaendelea kusimamia hoja isiyo kweli. Katika hali kama hii siwezi kuita kwamba ulikosea bali naamini uliamua kudanganya kwa makusudi. Naomba kwa mara ya pili, toa ushahidi ama kiri kwamba ulikosea.
Nimemaliza Tambaza 2001 hivyo matokeo yangu ni rahisi tu kuonekana baraza.Go and check Chinga, acha ubishi usio wa lazima. Kama kuna mtu anataka kujua kwamba kwanini nilipata A saba O-level, na kuendelea kushika nafasi ya kwanza Tambaza lakini Mtihani wa Mwisho nilipata daraja la pili niko tayari kujibu.
3. Ni kweli nimechelewa kumaliza shahada yangu ya utawala wa biashara(BBA) chuo kikuu cha DSM. Niwaombe radhi wote mnanionitakia mema. Najua suala hili linawaumiza sana. Suala hili lina muumiza zaidi mama yangu. Na hivi karibuni limekuwa sababu mojawapo ya mpenzi wangu ‘kuniacha '. Kwa hiyo nakiri kuwa ni changamoto. But time kills, time heals, Time tells. Niwaeleze tu context, si kwa nia ya kujitetea or justifying, ila kwa nia ya kuweka kumbukumbu sahihi.
Mzee Es, ni kweli ulilizungumza hili BCStimes. Na nikakujibu very boldly. Nilikuwa najua ninachokisema. Nimeshamaliza miaka mitatu ya kwanza kwa hiyo bado mwaka mmoja ambao una semester mbili. Moja ya darasani pamoja na mitihani, moja ni nje ya darasa bila mitihani(project work). So wakati ule nilikuwa naingia kwenye uchaguzi then mara baada ya uchaguzi ningefanya mitihani.
Lakini si kila ambacho unapanga wakati wote kinakuwa kama ulivyopanga, baada ya kifo cha Mzee Jumbe(RIP), uchaguzi ulisogezwa mbele na kuingilia mitihani-so I had two option- Ama kuacha kampeni na kujiandaa kwa ajili ya mitihani na kufanya mitihani au kuendelea na kampeni na kuahirisha masomo. Kupanga ni kuchagua. By then tayari watu wa Ubungo walikuwa na hamasa kubwa na tayari kuna wengi waliokuwa wameathika kwa namna moja au nyingine kutokana na kuniunga mkono. Sikutaka kujipendelea mwenyewe na kufanya usaliti. I had to swallow a difficult pill.
Nikawasilisha barua ya kuahirisha mwaka. Sasa nasuburi semester zangu ambazo sijafanya nirudi masomoni pamoja na kufanya viporo vya mitihani. Kwa hiyo toka Januari nimekuwa huru pindi nitakapokamilisha taratibu nitarajea. ( I hope hakutakuwa na siasa katika taaluma!). Ila nawashukuru wote kwa kuwa concerned. It's a valid concern. Mwanasiasa,umesema kweli kwamba nimewapa fursa wapinzani wangu ya kunishambulia.
Nakubaliana nawe. Lakini ni mashambulizi ya muda. Kwa upande mwingine, hata lisingekuwepo hili wangesema mengine, mashambulizi ni kitu cha kawaida kwa wanaoamini siasa za kimakaveli( mimi siamini katika the prince, naamini katika the new prince ya Dick Morris). Niliwasoma wote hawa kabla ya kuingia siasa. Visome vyote utajua ninachomaanisha. Soma pia kitabu cha Ashcroft-Dirty times, dirty politics utajua ninachokisema.
4. Swali linaloweza kuzuka ambalo ki msingi niliwahi kudokeza huko nyuma kwamba ilikuwa ni moja ya sababu kwa nini mama yangu ina particular alikataa kata kata nisigombee mwaka 2005 ni ‘kwa nini usisubiri kabisa ukamaliza ndio ukaingia siasa na kugombea?'. Narudia tena jibu nililomjibu-nilimwambia wakati huo nikiwa na miaka 24- ‘Nia ninayo, sababu ninazo, uwezo ni nao. Kwa nini nisubiri. Hivi kama kila mzazi akimwambia mwanae asiingie upinzani mtoto wa nani atakuwa upinzani. 2005 kuna uchaguzi, nataka ni-make a point kwamba vijana ama viongozi wa kizazi kipya tunaweza.
Nimewahimiza vijana walionizidi umri kugombea naona wengi wanaogopa. Nitawaonyesha kama inawezekana halafu chaguzi zijazo watajitokeza wengi zaidi. Sitaweza kutoa mfano huu vizuri kama nikisubiri mpaka mwaka 2010 ambapo nitakuwa na miaka 30. Najua hofu yako ni kuwa CCM watanifanya nisimalize masomo. Remember, nitakuwa na miaka 26 baada ya kumaliza uchaguzi. Nina muda bado wa kutosha wa kurekebisha historia.
Na wakifanya hivi watakuwa wametengeneza missile. Hii ndiyo maana ya struggle. Lazima kuna kafara kidogo. La muhimu ni kuhakikisha tu haiwi kafara kabisa ambayo hupoteza nguvu ya mapambano. Inawezekana. Wakati utathibitisha'. Inawezekana kuna majibu nimeyaruka katikati lakini hiyo ndiyo context! Samahinini wote mnaonipenda kama msimamo wangu unatazama zaidi umma na kusahau maisha binafsi. Mkitafakari kwa makini maneno yangu mtaona nimezingatia yote mawili.
5. Kuna mengi yamepotoshwa in between. Kwamba nashauriwa vibaya, infact mngesema najishauri vibaya kwa kuwa kila anayenizunguka ikiwemo ndani ya CHADEMA wanamsimamo kama wenu. Infact watu kama Eric Ongara huwa wananitukana kabisa katika hili. Kwa hiyo kama ni ushauri mbaya then najishauri mwenyewe vibaya.
Na ikizidi sana nawaruhusu kuniita ‘HAAMBILIKI'. Napokea ushauri wenu na kuufanyia kazi lakini nami pia najua ninachokitaka. Imesemwa kuwa posho za safari za CHADEMA ndio zinanipumbaza. Inachekesha!. Yoyote anayenifahamu hawezi kusema kauli kama hii. Uliyetoa hoja hii jua kwamba nasafiri zaidi ndani na nje ya nchi kwa shughuli zangu za nje ya chama zaidi ya za kichama.
Na ukweli ni kuwa financial napoteza kupindukia kwa kufanya kazi za CHADEMA. Both real(in terms of giving out) and opportunity(in terms of time) costs. Unayetoa hoja hii hebu pitia kidogo CV yangu. Nikupe mfano mdogo tu, wakati nikiwa consultant wa mradi wa kuwajengea uwezo wabunge nilikuwa nalipwa dola 100 kwa siku. Hii kufuru ukilinganisha na mshahara wa mwalimu wa Tanzania kwa mwezi. Siku hizi nimepunguza idadi ya siku za kazi zangu zingine kwa ajili ya chama.
Ni majitoleo ya kutosha. Niliamua kujitolea mwaka huu kwa ajili ya CHADEMA, mwakani pia nitajitolea kwa ajili ya chama. Nia nikujenga systems hususani ya vijana!(ili hata ukipunguza nguvu wawepo wengine wa kuendeleza). Halafu nitakwenda kujiendeleza zaidi kielimu. Nimejitolea kujenga chama mbadala Tanzania. Katika Maslow Hierarchy of needs mimi nimeshapita level ya basic needs. Siasa hainilishi wala kunivisha!.
6. Kwamba mimi na CHADEMA hatutoi kipaumbele kwa elimu. Another kichekesho!. Aliyesema hoja hii asome sera ya elimu ya CHADEMA. CHADEMA ni zaidi ya Mbowe na Mnyika, CHADEMA ni asasi ya watu wengi.
Infact siku moja nilipata shock mwaka jana mtu aliponiambia kwamba CHADEMA ni chama cha wasomi, makamu mwenyekiti katibu mkuu wote ni madaktari wa kusomea sio udaktari wa heshima na akanitupia lawama kwa nini mmnamuacha Profesa Baregu asimamie masuala ya kisera wakati kwa usomi wake wananchi hawatamwelewa.
Hili nitalijadili wakati najadili uhusioano wa CHADEMA na conservative. Umewahi kujadili elimu ya wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA kwa uwiano na kulinganisha na vyama vingine?. Nilisoma gazeti la mtanzania nikashangaa katika habari yake yake kuu kaburu alipojitoa sababu kuu iliyotolewa ni kwamba CHADEMA inakumbatia vijana wasomi.
Natambua umuhimu wa elimu. Yoyote anayetaka kujua msimamo wangu kuhusu elimu asome mada yangu niliyoandika nikiwa kidato cha sita na kuiwasilisha kwenye warsha ya wabunge Dodoma(Towards a more functional education in Tanzania). Knowledge is power.
When I said education makes a wise wiser and a fool more foolish Kikwete wakati huo akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje alisimama kupongeza ingawa alinilaumu kwa kuingiza issue ya Michael Sikupya kwenye mada yangu, Mwanri wakati huo akiwa Mbunge wa siha yeye alisifia approach ya ukombozi wa fikra.
Cheti ni muhimu lakini elimu ni zaidi ya cheti! That's is why as an emerging enterpreneur my first investment is in education in one of the district that is backward in this important sector. Anyway, yapo mambo mengi. Niache kwa sasa kuhusu CHADEMA na elimu yangu unless kama kuna maswali.
Nataka sasa kuingia kwenye suala la CHADEMA na conservative, then nitakuja suala la allegation za ukabila katika viti maalumu CHADEMA, then nitajadili allegation the CHADEMA kuwa ni business family, suala la helikopta, uhusiano wa CHADEMA na conservative then on and on mpaka nitakapo exhaust masuala yote!
Lakini kwa upande mwingine-nilishangaa kabisa mmeacha kujadili masuala mengi ya msingi katika lile tamko la EALA(tembelea
www.chadema.net, tazama pia katuni ya wiki icheke!). Naomba kila mmoja alipitie tena, tunapaswa kutazama zaidi maslahi mapana ya kitafa….
Coming soon………
Natabaruku.
JJ