Ama kweli kupambana na mafisadi kunahitaji kuwa na moyo wa chuma.
Nani anataka kuamini kuwa ujumbe huo umeandikwa na wanachadema?
Naona hoja za ufisadi zimekuwa nzitto kiasi kwamba hawa jamaa sasa wanafanya character assasination na watakia kazi njema ila tunahitaji majibu juu ya ufisadi .
Huyu Mbowe ambaye mahakama haimkamati amekuwa mkapa?ama analindwa na katiba ?
Haya kazi kwelikweli naam kumekucha , na mafisadi na vibaraka wao hawana pa kwenda kwa wakati huu ila ni mpambano mapka kieleweke.
Nahitaji ushahidi wa maneno mazito kama haya kwani huu sasa kama sio udaku basi ni udadaku....
Unajua kwa nini Slaa aliamua kuwataja hao anaowaita mafisadi kwa majina?. ili kuihabarisha jamii kuhusu hao anaosema ni mafisadi ili jamii ikiwezekana iwaelewe na iwe macho nao.
Angeamua angesema kuna wizi benki kuu, shilingi kadhaa ,cheki namba kadhaa.... halafu akamaliza mkutano kisha akaondoka
watu wangesema na kusema kuhusu huo ufisadi,lakini wasingewajua Hao wanaoitwa mafisadi na mwisho watu wangesahau mapema na wengine wangempuuza.
Ni vigumu kuelezea hoja from nowhere bila kuwa na mfano halisi wa kujengea hoja. kwa hiyo hata hilo suala la ufisadi Wapinzani wanaeleweka kwa sbabu wanakuja na figure halisi na wahusika halisi.
Hali hiyo ni sawa na Ufisadi huu wa maadili, Iwapo utamuonea haya mtu anayetembea na wake/waume za watu bila shaka hoja yoyote ya kukemea ufisadi-ngono itakuwa haina uzito sana.
Kwa hiyo, wacha waheshimiwa wanywe shubiri kwa niaba ya jamii, ili jamii wanayoiongoza ipone,
Otherwise na mapambano haya ya UKIMWI ambayo wanayaongoza/tunayaongoza hayawezi kupiga hatua yoyote ile,
Wakuu Heshima Mbele,
Binafsi I am very disturbed na yaliyojiri in general na hii topic, maana ndio kwanza nimeiona muda sio mrefu, uliopita.
That is all I can say for now, ninatka kuisoma yote kwanza, and then I will speak my mind kama kawaida.
Mbowe na Slaa waanza kuchokonolewa
*Waraka wasambazwa kwenye mtandao kuwachafua
*Ziara za Mwenyekiti za mikoani zatumiwa kummaliza
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huenda kikakumbwa na mtafaruku mkubwa, iwapo taarifa zinazosambazwa katika mtandao wa intaneti kuhusiana na uongozi wake wa juu hazitadhibitiwa na hatimaye kuaminika.
Katika hali isiyo ya kawaida, ndani ya chama hicho ambacho kimejizolea sifa ya kuwa na viongozi vijana na 'wapiganaji' katika ulingo wa siasa, kumezuka kundi la wanaojiita 'Wanamabadiliko CHADEMA' ambao wanadai kutaka kukisafisha chama chao.
Katika taarifa zao mbili tofauti katika mtandao wa intaneti, wanamabadiliko hao wanaushambulia uongozi wa juu wa chama hicho akiwamo Mwenyekiti Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Wilbroad Slaa.
Kuhusu Bw. Mbowe tuhuma hizo zinaelekezwa katika masuala ya kisiasa, kibiashara, kimahakama na kijamii, huku kwa Dkt. Slaa yanahusiana zaidi na masuala ya imani za kidini na maisha kijamii.
Wanadai kuwa wanachama wa CHADEMA wanawajibika kufanya mabadiliko ya uongozi, ili kukipa mwanga zaidi chama hicho ili uongozi wa sasa usije kuwa shabaha nzuri ya kumalizwa na wanaowaita mafisadi.
Waraka huo unamrudisha nyuma Bw. Mbowe katika kampeni za chama chake zilizofanyika Singida Mjini mwaka juzi, ambapo inadaiwa kwa sababu zake alishindwa kumsimamisha jukwaani mgombea ubunge wa chama hicho kujieleza na hivyo kushindwa kirahisi na aliyekuwa mgombea wa CCM, Bw. Mohamed Dewji.
"Kwa wanaobisha wakatazame kanda ya video ya mkutano wetu, pale Singida waone kama mgombea wetu alitambulishwa, la sivyo, Mbowe atoe maelezo kwenye Kamati Kuu," inasema sehemu ya waraka huo.
Mwenyekiti Mbowe pia anahusishwa na masuala mbalimbali kati yake na familia ya mmoja wa viongozi waandamizi ndani ya CHADEMA, ikidaiwa kuwa ulisababisha mtafaruku mkubwa hadi mahakamani na kumalizwa huko.
Lakini pia waraka unazungumzia ziara ya kiongozi huyo Newala na Nachingwea, ambako alifuatana na baadhi ya viongozi wenzake, huku ukionesha kugubikwa na dosari.
Pia unazungumzia ziara yake ya kichama eneo la Kawe, Dar es Salaam, ambayo pia ilisababisha mtafaruku kuhusiana na kikundi cha sanaa kinachomilikiwa na chama hicho, kiitwacho Malongo Sanaa Group.
Katika kile kinachoonesha ni kutaka kumchafua Mwenyekiti Mbowe, waraka unazungumzia pia ziara yake ya Zanzibar na Lindi na wilayani Hai, alikokuwa Mbunge kabla ya kuacha na kugombea ubunge na kuingia katika kinyang'anyiro cha urais.
"Kwa hiyo wanachama wenzetu, baadhi yetu sisi wa matawi ya mikoa ya Ruvuma, Dar, Kigoma, Manyara, Shinyanga na Arusha, tumeamua tuangalie mwelekeo wa mbele zaidi wa chama chetu.
"Mnyika (John) na Kabwe (Zitto) wanafanya kazi nzuri sana za kurecruit (sajili) vijana wenzao wasomi kwenye chama chetu. Wameanzisha mtandao wa vijana, ambao una matumaini ya kutuvunia wanachama na viongozi wasomi makini kwa siku za usoni," inasema sehemu ya waraka huo na kumalizia kwa kaulimbiu maarufu ya Bw. Mbowe ya 'Mpaka Kieleweke'.
Wakati huo huo, kutoka Dodoma, John Daniel anaripoti kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe, anatarajia kumaliza 'kifungo' chake Novemba 16 mwaka huu.
Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta aliwaambia wabunge jana asubuhi, kuwa Novemba 17 mwaka huu, Bw. Kabwe ataruhusiwa kuingia katika vikao vya kamati za Bunge kutokana na kuwa hataweza kuingia bungeni kutokana na mkutano wa tisa ulioanza jana, kuwa umemalizika wakati huo.
Kuhusu Mbunge huyo kutopewa rasmi barua ya kusimamishwa kwake shughuli za Bunge, Spika alisema si lazima Mbunge anayepewa adhabu kupewa barua, badala yake kanuni za Bunge hujitosheleza.
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4388
unaona wanatoa "huku".. watu wanakesha hapa unafanya mchezo..
mtoto wa mkulima, hivi inakuwaje kama mtu aliyeandika email hizo anazipanda JF, halafu anazinukuu kutoka JF na kuziweka kwenye magazeti yake? NIliposema wanakesha huku nina maana hao watu wa magazeti...
Hapo ndipo sie watu wa pwani tunapopenda mchuzi ulokolea ndimu na pilipili ya kutosha!!!!..................mtoto wa mkulima nakutakia mchana mwema huko 'mashariki ya mbali.'!!!!. Mkjj sio kwamba watu wanakesha, ila watu wanafanya home zao kwa ku-utilize resources zote available, which I think is great ingawa sikubaliani nao. Na hiyo isiwe sababu ya kutufumba sisi midomo yetu!!!.
Asante.
mtoto wa mkulima, hivi inakuwaje kama mtu aliyeandika email hizo anazipanda JF, halafu anazinukuu kutoka JF na kuziweka kwenye magazeti yake? NIliposema wanakesha huku nina maana hao watu wa magazeti...