itagata
JF-Expert Member
- Sep 4, 2011
- 210
- 71
SEKRETARIATI ya ajira ilipoanzishwa moja ya lengo lake ilikuwa ni kuajiri watu wenye sifa ikiwa ni pamoja na kupunguza urasmu uliokuwa ukitokea wakati taasisi zinazojitegemea na mamlaka za serikali za mitaa zilipokuwa na jukumu la kuajiri watumishi wake.
Pamoja na malengo hayo mazuri, hali imekuwa tofauti sana na ni afadhar mamlaka za serikali za mitaa pamoja na taasisi zinazojitegemea zilipokuwa na mamlaka ya kuajiri wafanyakazi wake, hali ilivyo sasa katika sekretariati ya ajira ni mbaya, bila kujuana au kutoa kitu kidogo usitegemee kupata kazi, imekuwa ni dili kubwa kwa ma-HR waliopo hapo na wenye jukumu la kuajiri.
Ninachojiuliza jamani wana JF kweli hadi Afisa Mtendaji wa Kijiji anasafiri kutoka Kigoma kuja Dar kwa ajili ya kufanya interview? Mi napingana sana na utaratibu huu kwani tunaoumia wengi ni watoto wa masikini tunaoka mikoa ya mbali na Dar.
Kwanini serikali isizipe na kuimarisha mikoa ili iweze kuajiri wafanyakazi wake badala ya kutegemea makao makuu ya secretariat pekee? Kama ni lazima utumishi waendelee kuajiri basi wachague baadhi ya kada angalau zenye vyeo vya juu ili wafanyakazi wenye vyeo vidogo waajiriwe na mamlaka za mikoa badala ya wote kutegemea kufanyiwa usaili na makao makuu ya utumishi.
Nina amini kuwa sisi watoto wa masikini tuliomaliza vyuo vikuu ambao hatuna uwezo wa kuhonga milioni moja ili tupewe kazi na tunaochangiwa na kijiji ili tupate nauli ya kuja Dar kufanya usaili ndio tunaoumia.
Nawaomba wapiganaji wetu, Zitto, Mbowe, Tundu, Mnyika na wapiganaji wengine wenye mapenzi mema na maisha ya vijana walipigie kelele hili ili angalau interview ziwe zinafanyika kwa ngazi ya kanda au mikoa ili kuwapa fursa watoto wa masikini kupata ajira.
Nimeamua kuandika mawazo yangu haya kwenu wana JF kwani nimefanya interview 3 ambazo nina uhakika nilifanya vizur lakini mpaka leo sijapata hiyo ajira, na ninatoka mikoa ya mbali nalazimika kusafiri siku mbili ili kufika Dar.