Mi ni mgeni wa Jamii forums naomba mnisaidie malalamiko haya yafike kunakotakiwa..
Ni muhitimu wa chuo cha uuguzi cha yohana wavenza kilichopo wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe.
Naandika malalamiko haya ili yaweze kuwafikia wanaohusika na kuweza kuyatatua maana mimi binafsi nimekuwa muhanga wa maovu haya na mpaka sasa bado yanaendelea huko chuoni.
Baadhi ya staff wenye nyazifa za juu chuoni hapo(Majina yao nayahifadhi) wamekuwa wakitumia nyazifa zao kuwanyanyasa kijinsia mabinti wanaochukua mafunzo chuoni hapo na kuwataka kingono haswa katika vipindi vya mitihani na vipindi vya kuripoti chuoni katika ukusanyaji wa ada na michango mingine..
Kuna mmoja ambaye yupo ngazi ya juu sana amekuwa na tabia ya kushinikiza utoaji wa mimba kwa baadhi ya wanafunzi wanaokuwa wamepata ujauzito aliosababisha yeye mwenyewe.
Staff wamekuwa na lugha chafu hadi kwa wazazi haswa kwenye suala zima la pesa na michango mbalimbali Hawasikiliza malalamiko yoyote yale na sababu za msingi mfano wazazi wamepitia kipindi kigumu cha ugonjwa wa corona kwa mwaka huu lakini still wanatolewa lugha chafu.
Wasimamizi wakuu wa chuo hicho wa jimbo la moravian wamekuwa wakifumbia macho malalamiko hayo kwa muda mrefu sasa na wanaoumia ni wazazi na wanafunzi wa chuo hicho.Mpaka sasa ninavyoripoti hali ya chuo sio shwari kwa ujumla hakuna maelewano kati ya wanafunzi na staff na inapelekea mahali hapo kutokuwa na hali salama ya kujifunza kwa wanafunzi..Naomba sana taasisi zinazohusika na mambo haya zisaidie kuokoa jahazi hili ili wanafunzi waweze kupata elimu stahiki pasipo kuathiri future zao.