cnjona
JF-Expert Member
- Mar 24, 2014
- 1,027
- 239
MSHAMBULIAJI Geilson Santana Santos ‘Jaja' kutoka Brazil Amewasili leo kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam.
kama kocha Mkuu, Mbrazil mwenzake, Marcio Maximo atamkubali, atafanyiwa vipimo vya afya ambavyo akifaulu pia atasajiliwa.
Na Yanga SC inataka kumuengua mshambuliaji Mganda, Emmanual Okwi katika usajili wake ili Mbrazil huyo achukue nafasi.
.
Yanga SC ina wachezaji watano wa kigeni kwa sasa bila ya Jaja na kabla ya kumtema Okwi, wengine wakiwa ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima wote wa Rwanda, Hamisi Kiiza na Coutinho.
Jaja aliyezaliwa Septemba 21 mwaka 1985 (Miaka 28) mjini Aracaju, Brazil anatokea klabu ya Itabaiana aliyojiunga nayo mwaka 2006 na kabla ya hapo alichezea klabu za Coritiba, Catuense, Olimpico, zote mwaka 2013, Maruinense, Lagarto mwaka 2012, Olimpico tena 2011, Domingos 2010, Confianca 2008 na Sergipe 2007.
Mbali na Maximo na Coutinho, kocha Msaidizi wa Yanga SC, Leonardo Neiva pia ni Mbrazil ambao wote wanaingia msimu huu.
===========================