Mbu wa Dar ni mdebwedo

Mbu wa Dar ni mdebwedo

Swahili AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
10,174
Reaction score
89,364
Mbu wa Dar wanatongoza kabla ya kung'ata uatasikia nzuuu nzuuu nzuuu, ukiwapush wepesi kinoma, dawa za kuchoma tu wapo hoi bin taabani.

Mbu hana afya kabisa.....
Mbu mwembamba kama sisimizi......
Mbu kakondeana kwa utapiamlo mkali.....
Mbu anahitaji msaada wa haraka ICU direct..
Malaria yao ukinywa maji mengi tu inaisha chap!
Mbu iking'ata kama inafanya massage

Njoo huku Kyela ukutane na
Mbu imeshiba
Mbu haitongozi, ni ming'ato tu
Mbu zinanyanyua net ndio zinaingia

Mbu unachoma dawa bado zipo ngangari kama Gen Z kule Kenya.
Malaria 🦟 yake bila sindano ya Artesunate hutoboi.
Mbu ukimpush ni mzito na ndo umemtia hasira
Mbu ukikutana nae unampisha kama binadamu.

Mbu akikung'ata haachi kipele anakuachia nundu kama za Mandonga akichezea kichapo
Mbu akikuchoma kama umechomwa na sindano 10cc yenye penadu. Lazima upake kishoka au diclogel kupunguza maumivu.

Mbu akikunyonya damu ni kuanzia robo lita ndo anakuacha.
Mbu inaweza beba mtoto na ikasepa nae.
Akiwa anapaa utazani umewasha feni panga boi

Kiufupi MBU wa Kyela sio wa mchezo mchezo wanajua kusudi la uwepo wao hapa duniani.
images (1).jpeg
 
Hao lazima wawe ngangari mkuu si majaruba ya mpunga mengi kwa hiyo wana makazi ya kutosha huku wanakondeana maana vichaka hakuna kwa hiyo makazi ni shida, msosi wenyewe wa manati maana watu wana makazi bora mixer fumigation kwa hiyo anapigwa vita ya kutosha wanaosurvive ndiyo hao wanakuwa mkondefu
 
Kuna ukweli nikiwa dar niking'atwa na mbu siugui malaria ila nikiwa Kwa M7 Kila baada ya wiki mbili malaria natetemeka nafuu kuipata Kwa drip nikipona nimeze sp kuzuia Kwa mwezi ni mateso
 
Mwanaume hata lotion haujawahi kuipaka mwilini ika lainisha ngozi, umekuja dar unajipaka mafuta ya mchikichi kama Sato wa kukaanga.

Hivi mbu wa Dar kweli aje kukugata na hio miharufu ya Sato, mbu wa Dar anakula ngozi laini tu inayokula chipsi kuku.
 
Back
Top Bottom