Mbu wameielemea familia yangu, Malaria haiishi nyumbani,kero ya kung'atwa imetuchosha

Mbu wameielemea familia yangu, Malaria haiishi nyumbani,kero ya kung'atwa imetuchosha

Mshua's

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
804
Reaction score
553
Wakuu habari zenu?

Mbu nyumbani kwangu wamekithiri kiasi kwamba ugonjwa wa Malaria hautibiki ukaisha kabisa. Vilevile kero ya kung'atwa na mbu kila mahali tukiwa nyumbani vimetuchosha, tunaomba msaada wa kuwaangamiza mbu hawa!

MAZALIO YA MBU
Yapo katika shimo la choo, mbu hutoka kupitia sinki la choo na kuenea nyumba nzima. Mazingira ya nyumba yoko safi kwa nje.

JITIHADA ZA KUZUIYA
Nimeweka mapazia ili kuzuiya mbu wasiingie moja kwa moja madirishani na milangoni. Hupulizia dawa aidha Expell au Hit, siku hiyo huwa shwari lakini kesho yake tatizo linarudia. Pia hutumia vyandarua.

Mwenye njia mbdala naomba atusaidie ili tuepukane na tatizo hili.
 
Badili Choo jenga cha kisasa kinachozuia harufu na mengineyo kutoka,au mwaga dawa ktk hilo shimo la choo.zipo dawa nyingi tu
 
Badili Choo jenga cha kisasa kinachozuia harufu na mengineyo kutoka,au mwaga dawa ktk hilo shimo la choo.zipo dawa nyingi tu

Mkuu choo ninachotumia ni kile cha kumwaga maji au wengine huita choo cha sinki, choo cha kukaa si kizuri kwa watu wengi na sipendi kutumia. Kuna choo cha kisasa zaidi ya hivi nilivyovitaja? Pia, naomba unitajie majina ya dawa za kumwaga kwenye mashimo ya vyoo ili nikanunue.

Kwa yeyote anayefahamu hizi dawa naomba atufahamishe
 
Nenda duka la kuuza pembejeo na madawa mifugo utakuta dawa mbali mbali kuna moja ya unga unga unatia maji unamwaga. Hadi mende wanaisha.
 
Back
Top Bottom