saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Wilaya ya Mbulu ilianzishwa mwaka 1905 wakati huo mfumo wa utawala ukiwa wa majimbo na wilaya. Mbulu ilikuwa mojawapo ya wilaya 2 ktk iliyokuwa jimbo la kaskazini iliyokuwa na wilaya za Arusha na Mbulu yenyewe.
Wilaya ya Mbulu ni mojawapo ya wilaya zilizo ktk maeneo yenye rutuba kubwa. Wilaya ya Mbulu ya wakati ule leo imegawanyika ktk wilaya za Hanang, Babati, Karatu na Mbulu yenyewe. Ingekuwa uzazi Mbulu leo ni babu lakini je ni kwa bahati mbaya makao makuu ya wilaya ya Mbulu mpaka leo hayajafikiwa na barabara ya lami?
Wilaya zilizozaliwa kutoka wilaya ya Mbulu makao makuu yao yameshafikiwa na barabara za lami muda mrefu. Mi nauliza Mbulu kuna nini mbona imepuuzwa hivi? Mh. Rais mwogopeni Mungu mnashindwa kweli kuwajengea hao wananchi Km 75 tu wakati mnajenga miradi ya mamia ya kilometa?
Ujenzi wa barabara ya Mnivata-Tandahimba-Newala-Masasi wa zaidi ya Km 160 umeshaanza. Mkataba wa ujenzi wa barabara tajwa ulisainiwa baada ya ule wa Karatu-Mbulu uliosainiwa tarehe 16.06.2023 lakini hakuna dalili ya kuanza ujenzi.
Jamani Mbulu kuna nini?