Hii inatokana na serikali yenye watendaji na viongozi fake wasio na ubunifu katika kutenda kazi zao, nguvu zaidi akili robo
Wajinga sana hao
Lazima sheria zifuatwe,sijaona nchi kama hii inayoongozwa kwa matukio
Mtu analalamikiwa ooh kuna maiti imeshikiliwa hospital na yeye kwa kujionesha eti haya ambulance iende ikambebe wakazike
Sasa ni uungwana lakini kwanini wasitatue hilo tatizo linalijirudia kila sehemu na kuifanyia sheria ya nchi nzima badala ya tukio na tukio?
Yule mama nae kakaa anasubiri mtoto auwawe au mwanamke adhalilishwe ndio anakurupuka kutoka ofisini na kutatua shida hiyo
Kama mdau humu alipoandika mada ambayo ilimfanya ajibu haraka
Angalia mwalimu aliehukumiwa kifo kisa kamchapa mtoto wa shule mpaka kafariki
Halafu hii inapita badala ya kupeleka bungeni na kuwa hoja ya siku nzima
Mwalimu anauwa kwa kupiga bado mnaruhusu kupiga shuleni kama sio upumbavu ni nini?
Mtu anazunguka kusubiri mwananchi atalalamika hana maji au umeme halafu anatatua hapo na kesi imeisha na huenda yakawa maneno tu ya mbele ya waandishi wa habari na akiondoka tu imetoka