Mbunge Agnesta Kaiza: Kesi za kubambikiwa zinasababisha mrundikano katika magereza

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge Agnesta Kaiza ametaja ubambikizaji wa kesi nyingi za jinai kuwa sababu mojawapo ya mrundikano katika magereza. Amesema hayo leo Bungeni Dodoma.

Amefafanua, "Kila leo unasikia fulani ana kesi ya Uhujumu Uchumi. Mke na Mume wakipigana nyumbani wakifikishwa Mahakamani unaambiwa umehujumu Uchumi".

Aidha, Mbunge huyo amesema uwepo masharti magumu ya upatikanaji wa dhamana pia inapelekea mrundikano katika magereza na mahabusu.

Ameshauri kupitishwa Sheria ya uwepo wa ukomo wa upelelezi kwa kesi zinazochukia muda mrefu akisema hilo likifanyika mrundikano usio wa lazima utapunguzwa moja kwa moja.
 
MwananchiHabari ZaidiKitaifa

Watu 243 wakiri makosa, walipa fidia ya Sh35 bilioni

WEDNESDAY APRIL 28 2021

makosapic
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Summary
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kiasi cha Sh35.07 bilioni kimepatikana baada ya washtakiwa mbalimbali kukiri makosa.

New Content Item (1)By Sharon Sauwa
More by this Author

Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kiasi cha Sh35.07 bilioni kimepatikana baada ya washtakiwa mbalimbali kukiri makosa.

Profesa Kabudi ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 28, 2021 wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema wizara kupitia ofisi ya Taifa ya mashtaka imeendelea kutekeleza zoezi la makubaliano ya kumaliza kesi za jinai chini ya utaratibu wa washtakiwa kukiri makosa yao kwa mujibu wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 11 ya mwaka 2019.

Amesema katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021, kesi 192 zilihitimishwa kwa njia hiyo.

Amesema jumla ya washtakiwa 243 walikiri makosa na kulipa serikalini kiasi Sh35,07 bilioni kama fidia pamoja na faini kutokana na makosa ya uhujumu uchumi.

Siamini kama hawa walikiri kwa hiari zao.

Huwezi kumuweka mtu kizuizini miaka kadhaa bila dhamana, halafu utake maongezi nae akatae.

Hii sheria ni kandamizi.
 
Alikuwa wapi wakati yule kenge anazitumia hizo kesi komoaji kuumiza Watanzania.
 
You keep on complaining while the powers to make changes are on your finger tips! Hizi sheria za kipuuzi si mlizipitisha kwa nderemo na vifijo humo humo Bungeni? Mnalalamika nini while you are part of the problem?
 
MwananchiHabari ZaidiKitaifa
Watu 243 wakiri makosa, walipa fidia ya Sh35 bilioni
WEDNESDAY APRIL 28 2021

makosapic
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Summary
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kiasi cha Sh35.07 bilioni kimepatikana baada ya washtakiwa mbalimbali kukiri makosa.

ADVERTISEMENT
New Content Item (1)By Sharon Sauwa
More by this Author

Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kiasi cha Sh35.07 bilioni kimepatikana baada ya washtakiwa mbalimbali kukiri makosa.

Profesa Kabudi ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 28, 2021 wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema wizara kupitia ofisi ya Taifa ya mashtaka imeendelea kutekeleza zoezi la makubaliano ya kumaliza kesi za jinai chini ya utaratibu wa washtakiwa kukiri makosa yao kwa mujibu wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 11 ya mwaka 2019.

Amesema katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021, kesi 192 zilihitimishwa kwa njia hiyo.

Amesema jumla ya washtakiwa 243 walikiri makosa na kulipa serikalini kiasi Sh35,07 bilioni kama fidia pamoja na faini kutokana na makosa ya uhujumu uchumi.

Siamini kama hawa walikiri kwa hiari zao.
Huwezi kumuweka mtu kizuizini miaka kadhaa bila dhamana, halafu utake maongezi nae akatae.
Hii sheria ni kandamizi.
Huyu Kabudi anataka kuendeleza ule uhuni wa jiwe.Watu kurudisha hela na kukiri haimanishi walizila hizo hela watu wanataka uhuru maisha yaende.

MMEUMIZA WATANZANIA WENGI MNO KWA JINA LA HILI KESI LA UHUJUMU UCHUMI alafu anatokea mbuzi mmoja anasema ETI A REAL SON OF AFRICA hilo jina marehemu nani alimpa na hiyo kofia ya MTOTO HALISI WA AFRICA alivishwa na nani. Watu tuna machungu yetu ndugu zetu wamekufa na kiharusi kwa kufilisiwa wengine wamekuwa machizi.
 
Mbunge Agnesta Kaiza ametaja ubambikizaji wa kesi nyingi za jinai kuwa sababu mojawapo ya mrundikano katika magereza. Amesema hayo leo Bungeni Dodoma...
Hivi leo ndio wanaliona hilo,je wakati wakipitisha ile miswaada ya hati za dharura ,waliuona utamu wa posho za vikao vile.Walikuwa hawajui wanakulitafuta wanakulipata?
 
Huyu Kabudi anataka kuendeleza ule uhuni wa jiwe.Watu kurudisha hela na kukiri haimanishi walizila hizo hela watu wanataka uhuru maisha yaende.

MMEUMIZA WATANZANIA WENGI MNO KWA JINA LA HILI KESI LA UHUJUMU UCHUMI alafu anatokea mbuzi mmoja anasema ETI A REAL SON OF AFRICA hilo jina marehemu nani alimpa na hiyo kofia ya MTOTO HALISI WA AFRICA alivishwa na nani. Watu tuna machungu yetu ndugu zetu wamekufa na kiharusi kwa kufilisiwa wengine wamekuwa machizi.
Kati ya mawakala wa shetani hapa Duniani, huyu Kibudu ni mmojawapo. Huyu ni sehemu kubwa ya uovu uliofanywa na marehemu.
 
Back
Top Bottom