MwananchiHabari ZaidiKitaifa
Watu 243 wakiri makosa, walipa fidia ya Sh35 bilioni
WEDNESDAY APRIL 28 2021
makosapic
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Summary
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kiasi cha Sh35.07 bilioni kimepatikana baada ya washtakiwa mbalimbali kukiri makosa.
ADVERTISEMENT
New Content Item (1)By Sharon Sauwa
More by this Author
Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kiasi cha Sh35.07 bilioni kimepatikana baada ya washtakiwa mbalimbali kukiri makosa.
Profesa Kabudi ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 28, 2021 wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Amesema wizara kupitia ofisi ya Taifa ya mashtaka imeendelea kutekeleza zoezi la makubaliano ya kumaliza kesi za jinai chini ya utaratibu wa washtakiwa kukiri makosa yao kwa mujibu wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 11 ya mwaka 2019.
Amesema katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021, kesi 192 zilihitimishwa kwa njia hiyo.
Amesema jumla ya washtakiwa 243 walikiri makosa na kulipa serikalini kiasi Sh35,07 bilioni kama fidia pamoja na faini kutokana na makosa ya uhujumu uchumi.
Siamini kama hawa walikiri kwa hiari zao.
Huwezi kumuweka mtu kizuizini miaka kadhaa bila dhamana, halafu utake maongezi nae akatae.
Hii sheria ni kandamizi.