Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Mbunge wa Katavi, Thomas Kampala ametoa hoja bungeni leo, Septemba 4, 2026 katika wizara ya Habari sanaa michezo na utamaduni kuhusu maadili ya watoto wanaocheza shule za Academy za Mpira, bungeni Dodoma.
Thomas Kampala Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze serikali kwa kutoa miongozo ya maeneo mengi kutengeneza akademi za watoto na kwenye vilabu vyetu kuwa na timu za watoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa kuna malalamiko mengi kwenye akademi nyingi na vilabu vingi vya watoto.
Wale watoto kwenye zile akademi ili wapate namba, lazima waingiliwe kinyume na maumbile na makocha. Klipu hizo zimekuwa zikitembea sana kwenye mitandao.
Na je, Waziri unalifahamu hili? Na kama unalifahamu, serikali ina mpango gani wa kuchukua hatua maeneo ambayo vitendo hivi vinafanyika? Asante."
Waziri Makonda: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Kambaya ambaye amekuwa balozi wetu nguli wa maadili katika nchi wetu wa Tanzania.
Na kila mara tukimsikia, tunajua anazungumzia jambo la maadili. Na jambo hili analolizungumzia kwa kweli, Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la maadili. Kwa sababu kijana mwenye kipaji hapaswi kulipa au kutozwa fedha ili acheze, kipaji chake ndicho kinapaswa kutumika kama kigezo cha kumpanga na kumpa fursa ya kucheza.
Serikali inafuatilia, na tumetoa maelekezo mara kwa mara. Na tunajua vyombo vya serikali vipo na tutahakikisha ya kwamba kazi hii inafanyika vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikutolee mfano mmoja mdogo tu: Mechi ya Simba na Yanga ambayo huwa inafanyika Zanzibar kwenye Uwanja wa Amani, kwenye collection ya mapato tulikuwa tunapata milioni 40. Lakini maelekezo ya wizara tulivyoyatoa, mwaka huu mechi imechezwa kwenye uwanja ule ule tumepata takribani ya milioni 217.
Kwa hiyo unaweza ukaona matendo ya maadili haya hayako tu kwenye upande mmoja wa namba, lakini hata kwenye collection, kwenye attitude ya watu kupata fursa kwenye usajili.
Kwa hiyo serikali inaendelea kuweka mikakati thabiti ya kupanga na kuhakikisha kwamba tunaweka macho yetu yote ili tuwapate watu wenye vipaji, na ndani ya vile vipaji pesa ipatikane na taifa liweze kunufaika."