Mbunge Aida Khenani yuko wapi?

Mbunge Aida Khenani yuko wapi?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
10,448
Reaction score
8,705
Tangu CHADEMA wameanza kampeni zao za Chadema digitali hadi ya Katiba Mpya huyu Mheshimiwa sijamsikia. Viongozi na wanachama wenzake wanawekwa ndani lakini yuko kimya.

Mwenyekiti wake anafunguliwa mashtaka ya ugaidi bado yuko kimya. Lakini wakati haya yanaendelea anafungua mashindano ya Aida Cup akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Lijualikali.

Kwa mawazo yangu ni bora angetangaza kujitoa kwenye chama chake ili aweze kuwatumikia vizuri wananchi wa Nkasi ambao alisema walimchagua yeye na sio chama chake.

Baada ya kujitoa ajiunge na chama tawala ambacho bila shaka kitampa nafasi ya kugombea kiti hicho katika uchaguzi maalum utakaofuta.

Kwa vile chama cha awali hakitagombea (hata kingegombea) bila shaka atashinda na ataweza kuwawakilisha watu wa jimbo lake bila nafsi yake kumsuta. Kama ataona aibu kufanya hivyo, chama chake, kwa heshima na taadhima kichukue kadi yao ili awe huru.

Hivyo hivyo kwa madiwani wanaokiwakilisha chama hicho katika maeneo yao.

Amandla..
 
Chama kikiona ana kosa kimfukuze kama walivyofukuzwa hao mnaowaita covid19.
 
Chama kikiona ana kosa kimfukuze kama walivyofukuzwa hao mnaowaita covid19.

Yeye kama mwakilishi pekee wa chama chake bungeni alitakiwa kuonyesha kuguswa na magumu ambayo chama chake kinapitia. Kujifanya haoni wala hasikii sio ishara nzuri. Naona anatumia kivuli cha wale 19 kujificha.

Amandla...
 
Mh.Aida Khenan ni mzalendo Sana...ana tabia ya kuangalia mbali kwa maslahi ya wananchi na nchi.

Kama mmemchoka mfukuzeni uanachama tutamshawishi ajiunge nasi CCM.

#AidaNiMzalendo
#AidaAnajitambua
 
Msimlazimishe kuunga mkono mambo hayana tija. Yeye kipaumbele chake ni jimbo lake.
Hamna mtu anayemlazimisha. Yeye yuko bungeni kama mwakilishi wa Chadema na hivyo anawajibika kwa Chadema. Kama anaona mambo wanayofanya Chadema sasa hivi hayana tija ( ambayo ni haki yake ya msingi ) basi awe muwazi kwa kutofautiana nao hadharani au ajiudhuru ili apate nafasi ya kurudi kupitia chama ambacho dira yake anaikubali. Kama anakubali kuwa Mwenyekiti wa chama chake ni gaidi, ana sababu gani kubaki katika chama kinachoongozwa na gaidi?

Kukaa bungeni kwa kofia ya Chadema wakati hakubaliani nayo ni unafik wa hali ya juu. Atoke tuu, atarudi kwa asilimia 100. Ama kwa chama kingine au kwa Spika kukataa kutambua kujiuzuru au kuachishwa kwake. A

Amandla...
 
Mh.Aida Khenan ni mzalendo Sana...ana tabia ya kuangalia mbali kwa maslahi ya wananchi na nchi...

Sidhani kama itakuwa kazi ngumu kumshawishi ajiunge na chama chenu maana ameisha sema kuwa yeye maslahi ya wananchi wake ni zaidi ya mahitaji ya chama chake.

Sasa kama maslahi yao yatafaidika na yeye kuwa CCM, sioni sababu ya yeye kubaki Chadema. Bila shaka wananchi wa jimbo lake wataamuunga mkono. Na sidhani kama Chadema watasononeka kwa kuondoka kwake. Tena akihama anaweza kupata hata kaunaibu uwaziri.

Amandla...
 
Alishasema kuwa covid 19 akiwa bungeni wanamkebehi,pia akasema hajawahipewa taarifa yoyote kutoka chadema kuhusu uhalali wake wa ubunge.

Alijibiwa kuwa hakuna kikao chochote kimewahi kumjadili yeye.

Hivyo kufanya kazi jimboni kwake ni sahihi kabisa,issue zingine nikumchonganisha tu.
 
Tangu CHADEMA wameanza kampeni zao za Chadema digitali hadi ya Katiba Mpya huyu Mheshimiwa sijamsikia. Viongozi na wanachama wenzake wanawekwa ndani lakini yuko kimya...
Yupo mzima wa afya anachapa kazi! Unataka atoke aende wapi magomeni au kariakoo? 😀😃
 
Unataka aache kushughulikia kero za wananchi jimboni kwake aje ufipa kupiga porojo zisizo na tija? Yeye siyo katibu mkuu wala msemaji wa chama, unataka ajitie kimbelembele kukisemea chama kama nani?

Acheni upuuzi huo wa kudhani kuwa chama chenu ni muhimu kuliko familia au wananchi waliowachagua kuwawakilisha.
 
Alishasema kuwa covid 19 akiwa bungeni wanamkebehi,pia akasema hajawahipewa taarifa yoyote kutoka chadema kuhusu uhalali wake wa ubunge.
Alijibiwa kuwa hakuna kikao chochote kimewahi kumjadili yeye.
Hivyo kufanya kazi jimboni kwake ni sahihi kabisa,issue zingine nikumchonganisha tu.
Kwa nini hakusubiri maelekezo kutoka kwenye chama chake kabla ya kwenda kula kiapo cha ubunge? Alifanya hivyo akijua thika kuwa chama chake hakitambui uchaguzi uliompa yeye ushindi. Sasa sielewi anasubiri taarifa ipi? Kama hawajamjadili ina maana yeye bado ni mwanachama wa Chadema. Labda kama amewapigia private call.

Kufanya kazi kwake jimboni ndio kuna mnyamazisha kwenye masuala yanayohusu chama chake? Kama mwanachama anashindwa kweli kutoa tamko lolote kuhusu hali ya Mwenyekiti wake? Hata pole? Yeye kama mbunge ameruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara jimboni mwake, hivyo mtu ungetegemea angefanya mikutano qmbamo angezungumzia mambo ya chama chake k.m. Chadema Digitali n.k. Lakini kimyaaa

Amandla...
 
Unataka aache kushughulikia kero za wananchi jimboni kwake aje ufipa kupiga porojo zisizo na tija? Yeye siyo katibu mkuu wala msemaji wa chama, unataka ajitie kimbelembele kukisemea chama kama nani?
Acheni upuuzi huo wa kudhani kuwa chama chenu ni muhimu kuliko familia au wananchi waliowachagua kuwawakilisha.
Na wabunge wote wa chama chako wanaozungumzia ilani ya chama chao jimboni kwao ni wasemaji wa CCM? Na wanafanya hivyo kwa sababu chama chao ni muhimu kuliko familia au wananchi waliowachagua kuwawakilisha?

Kuna ubaya gani yeye kama mwanachama wa Chadema kuzungumzia ilani ya chama chake akiwa jimboni mwake? Anaogopa nini? Ingekuwa Chadema wana nia mbaya nae, wangemfukuza chamani kama ilivyokuwa kwa wakina Halima.

Mimi sioni sababu ya yeye kujificha na kujitenga na chama chake. Labda kama anaamini kuwa hakihitaji kwa sababu, kama alivyosema awali, alipigana mwenyewe mpaka akachaguliwa. Kama ni hivyo ni bora angeachana nacho kabisa.

Amandla...
 
Tangu CHADEMA wameanza kampeni zao za Chadema digitali hadi ya Katiba Mpya huyu Mheshimiwa sijamsikia. Viongozi na wanachama wenzake wanawekwa ndani lakini yuko kimya...
Hahaha kapoteana. Analipa gharama za ubunge wa kupewa. Waliompa akina Jiwe, Polepole na Bashiru Pembe zao zimekatwa. Hana mtetezi tena
 
Back
Top Bottom