Mbunge aliyedai waongezewe mshahara atakiwa aachie jimbo, CCM nao watoa kauli

Mbunge aliyedai waongezewe mshahara atakiwa aachie jimbo, CCM nao watoa kauli

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga kama anataka kuhudumia wananchi afuate utaratibu wa nchi na akitaka kulipwa kwa dola ahamie katika nchi zinazofanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aliopohojiwa na gazeti la Nipashe

Kwa upande wake kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala hilo alisema

Kama maslahi hayatoshi aache kazi ya Ubunge.

"Wabunge wasipoogopa wananchi hawatakuwa wabunge, Wakati Rais anawaambia wafanyakazi hawawezi kupandishia mishahara kwa sababu ya hali ya uchumi, Mbunge anataka malipo zaidi ni hujuma kwa Rais".

#Nipashe


FB_IMG_1624517732483.jpg
 
na akitaka kulipwa kwa dola ahamie katika nchi zinazofanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo
Chongolo anatakiwa kuwa na hekima Sana ktk kuwajibu wabunge wa chama chake. Huyu ni mbunge, ana hadhi yake. Hata kama hoja yake inaleta maudhi lkn Chongolo kwa nafasi yake hakupaswa kutoa majibu ya kidikteta kiasi hiki.

Tisizilee kauli za kibabe kiasi hiki.
 
Chongolo anatakiwa kuwa na hekima Sana ktk kuwajibu wabunge wenzake. Huyu ni mbunge, ana hadhi yake. Hata kama hoja yake inaleta mwudhi lkn Chongolo kwa nafasi yake hakupaswa kutoa majibu ya kidikteta kiasi hiki.

Tisizilee kauli za kibabe kiasi hiki.
Anzeni kugombana mwisho mtaanzisha chama kipya Cha siasa.
 
Watakuwa wamedukua mitambo yetu na kusikia kwamba tarehe 1 Julai tunaandamana nchi nzima ili kuwafurusha woooooooote Mjengoni pamoja na timu yote huko juu ya Bi Mkubwa wao.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Chongolo anatakiwa kuwa na hekima Sana ktk kuwajibu wabunge wa chama chake. Huyu ni mbunge, ana hadhi yake. Hata kama hoja yake inaleta maudhi lkn Chongolo kwa nafasi yake hakupaswa kutoa majibu ya kidikteta kiasi hiki.

Tisizilee kauli za kibabe kiasi hiki.
Kuleana ndiko kunakoliangamiza taifa, kwanini yeye hakutumia hekima kuomba nyongeza ya mshahara huku akijua mwalimu anapata laki 3 kwa mwezi wakati yeye anaipata kwa siku.
 
Huyu mbunge hakupaswa kuhukumiwa kwa hisia na machungu ya umaskini wetu. Alipaswa kupewa nafasi ya kufanya hata mdahalo wa wazi ili ajenge hoja yake, kisha apigwe maswali na kuyatolea majibu.

Ukiangalia wachangiaji wengi ktk nyuzi zinazohusu kauli ya huyu mbunge, hakuna anayepinga kwa hoja kuntu. Wengi wanajadili utofauti uliopo Kati ya mshahara wa mbunge na wafanyakazi wengine.

Lkn hawajikiti kwenye mantiki ya hoja ya mbunge kwamba mshahara haumtoshi mbunge ukilinganisha na majukumu aliyo nayo.
 
Back
Top Bottom