Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge Aloyce Kamamba: Mwanafunzi Aliyebeba Ujauzito Shuleni Ahudumiwe
Mbunge wa Buyungu, Aloyce Kamamba amesema mwanafunzi aliyepata ujauzito akiwa shuleni akirudi masomoni baada ya kujifungua sheria imuangalie upya namna ya kumhudumia kwa kumpatia elimu kwa kuwa anakuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kulea.
Kamamba amesema mwanafunzi huyo anapaswa kupewa uangalizi maalumu ili kumwezesha kufanya vizuri kwenye masomo huku akiendelea kumhudumia mtoto wake.
Kamamba amesema hayo akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa mwaka 2024/2025.