Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa) Anayetokea Kundi la Vijana Zanzibar, Mhe. Amina Ali Mzee ametembelea vituo mbalimbali vya Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar vinavyoandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kutokana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika 27 Novemba, 2024.
Mhe. Amina Ali Mzee Amewataka Vijana pamoja na wanachi wote Kwa ujumla Kujitokeza Kwa Wingi Kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Kupiga Kura ili kuwa sifa za kuweza kupiga kura kuchagua vingozi wanawaotaka wao wenyewe.
"Usipojiandikisha na usipoonekana kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura hutaweza kupiga kura kuchagua viongozi bora na pia hutaweza kugombea nafasi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Ni vyema wote kujiandikisha sasa" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa
Aidha, Mhe. Amina Ali Mzee amewasihi Vijana kujitokeza kushiriki uchaguzi kwa kuchukua fomu na kuwania nafasi mbalimbali zilizotolewa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuendelea kupikwa, kuwa wazoefu na kuwa viongozi wazuri wa baadaye.
Mhe. Amina Ali Mzee Ameyasema hayo tarehe 09 Oktoba, 2024 Alipotembelea Kwenye baadhi ya Vituo vya Kujiandikisha Kupiga Kura Mkoa wa Mjini Unguja.
Soma Pia: Waziri Mchengerwa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bara utafanyika 27 November, 2024