Pre GE2025 Mbunge Anne Kilango Malecela tunaomba utekeleze ahadi uliyoahidi kipindi cha uchaguzi kukiunganisha kijiji cha Lugulu na umeme wa REA

Pre GE2025 Mbunge Anne Kilango Malecela tunaomba utekeleze ahadi uliyoahidi kipindi cha uchaguzi kukiunganisha kijiji cha Lugulu na umeme wa REA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kunguu

Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
24
Reaction score
12
Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela, Wakazi wa Kijiji cha Lugulu chenye vitongoji vinne ambavyo ni Lugulu, Masheni, Ramu, na Mkondogwe, tunaomba utekeleze ahadi yako ulioahidi kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2005, 2020. Pia mwaka 2020 ulituhakikishia utapambana ili kuhakikisha Kijiji cha Lugulu kinaunganishwa na umeme WAREA. Wananchi wanalalamika sana kuhusu ahadi hii kushindwa kuitekeleza kwa muda mrefu.

Shule ya Secondary Lugulu imepatiwa computer, ila wanafunzi na walimu hawawezi kunufaika na msaada huu wa computer kama hakuna umeme. Tunaomba ahadi hii itekelezwe ili wanafunzi na walimu waweze kunufaika na computer hizi.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Mashaka Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Same, Meneja WAREA Kanda ya Kaskazini, Tunawaomba wakazi wa Kijiji cha Lugulu tupatiwe umeme maana ahadi hii ya kuunganishwa umeme Kijiji hiki cha Lugulu imekuwa ya miaka mingi bila utekelezaji.

Rais na Mama yetu Samia Suluhu Hassan amewaamini sana na kuwapa dhamana kumsaidia ili kutatua kero zinazowakabili wananchi, tunaomba kero hii ya kuunganishwa na umeme WAREA muifanyie kazi ili kuepuka malalamiko ya wananchi wa Lugulu.
 
Back
Top Bottom